SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mbunifu Linda Bezuidenhout Ametuambia Ilikuaje kumvalisha Mke Wa Rapper T.I
Mitindo

Mbunifu Linda Bezuidenhout Ametuambia Ilikuaje kumvalisha Mke Wa Rapper T.I 

Linda Bezuidenhout linaweza kuwa jina geni kwa wengi lakini kama ni mfuatiliaji wa mitindo huwezi kukosa kumjua, Linda ni chotara wa ki Tanzania na Dutch ni mbunifu ambae yupo katika ulimwengu wa mitindo kwa miaka 20 sasa. Linda kwa sasa anaishi Atlanta, ambapo bado anaendelea na kufanya ubunifu.

hivi karibuniLinda na kampuni yake ya LBC (Linda Bezuidenhout Couture) imefanikiwa kumvalisha mke wa Rapper T.I, Tiny Harris katika jarida la upscalemagazine 2017 Holidays issue.

Tumepata kuongea nae mawili matatu kuhusu kupata deal hii ambayo ni kubwa

Afroswagga – tungependa kujua ilikuaje mpaka ukaweza kumvalisha Tiny?

Linda –  Mimi ni Designer mkubwa hapa Atlanta mastar wengi wanatambua kazi zangu Alhamdulilah.
Kwahiyo walivotaka nguo ya couture na walitaka iwe ya Designer wa hapa hapa Atlanta wakurugenzi wa upscale magazine wakaja Linda Bezuidenhout Couture Boutique ndo wakaja dukani. Wakachagua nguo 3 Kati ya zile 3 hiyo ndo ilipendwa zaidi Tiny.

Afroswagga – baada ya kumvalisha deals zimeongezeka?

Linda – Ofcourse kumvisha mtu maarufu kama Tiny inatangaza brand yetu kwa kasi sana na kuongeza wateja Alhamdulilah
Kwa upande wa deals hizo uwa zina kuja kwa ghafla uwa ni mipango ya mungu na sio kwa ajili ya kumvalisha Star Alhamdulilah 🙏🏾

Afroswagga – Je unaplans za kufungua Linda Bezuidenhout Tanzania?

Linda – InshaAllah ntaanza na consignment store kwanza kujaribu soko. Yani ntafanya mkataba na Boutique yenye Adhi kubwa ili iweke LB dukani mwao na kawaida ya Consignment business mwenye duka atachukua asilimia 40 kwenye kila gauni litakalo uzwa. Tukiona soko zuri basi tutafungua brunch ya LB Tanzania InshaAllah
Yani mwenye duka hato nunua LB ntampa tu aweke dukani itakapo uzwa tutagawana mauzo wao watachukua 40% MIMI 60%

Kwa wenye maduka makubwa Linda ana wapokea kwa mikono miwili, sisi kwetu tunasema hongera Linda na endelea kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia ubunifu wako.

Related posts

2 Comments

  1. penis prosthetic big penis big prosthetic big dildo erect penis prosthetic

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mbunifu-linda-bezuidenhout-ametuambia-ilikuaje-kumvalisha-mke-wa-rapper-t-i/ […]

  2. dk7คาสิโน

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mbunifu-linda-bezuidenhout-ametuambia-ilikuaje-kumvalisha-mke-wa-rapper-t-i/ […]

Comments are closed.