SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mbunifu Sheria Ngowi Ni Mfano Mzuri Wa Msemo Nabii Hakubaliki Kwao
Mitindo

Mbunifu Sheria Ngowi Ni Mfano Mzuri Wa Msemo Nabii Hakubaliki Kwao 

Kwetu sisi ukiongelea mbunifu wa mavazi ya kiume ambae anahitaji kila aina ya heshima basi una muongelea Sheria Ngowi, Sheria is a legend & he will surely leave a legacy siku moja. Kuna ambao hamumjui Sheria ni nani labda kwa sababu tu kwa sababu ana fanya kazi yake iongee zaidi kuliko yeye mwenyewe, si mtu wa kiki havalishi models wanaojulikana mavazi yake ili kupata kiki. Tunaweza kusema Sheria ni kama Kobbe yupo slow but sure.

Wengine tunamjua kwa jina la Sheria Ngowi lakini jina lake halisi ni Walter Thomas Ngowi, Sheria Ngowi  ni brand name yake ambayo yeye ameikuza kupita jina lake na sio kutaka umaarufu wa yeye mwenyewe kuliko brand yake, kama ambayo tulisema katika vitu vya kuzingatia ili kuacha legacy katika tasnia hii ya mitindo kimoja wapo ni kukuza jina la bidhaa yako kuliko kutaka kujulikana wewe mwenyewe kuliko kazi yako.

Sheria kwa sasa ameshavuka kuitwa mbunifu wa kitaifa bali ni mbunifu wa kimataifa kwanini? Sheria ana show case collection zake nje ya Nchi na zinapokelewa vyema, ana unique taste katika bidhaa yake. Kitu ambacho utakiona kwa Sheria ni aghalabu kukiona kwa mtu mwingine tukiongelea materials na finishing za kazi yake.

Japokuwa hapa kwetu haongelewi sana lakini Sheria anaongelewa na magazeti makubwa ya mitindo Nje ya Nchi, gazti kubwa la mitindo GQ Italia walishawahi kufanya nae interview na kumuweka katika Gazeti lao, ilikuwa mwaka 2011 ana miaka mitatu toka anaanze kuwa mbunifu, na kuweza kutamuliwa  na gazeti kubwa kama hilo ambapo tunaweza kusema ni moja kati ya wabunifu wachache kutoka Africa Mashariki waliopata nafashi hio.

Tuzo! Tuzo! Tuzo! wanasema nabii hakubaliki kwao, au labda hapa kwetu ushindani ni mkubwa kuliko Nchi nyingine hatuwezi kuhesabu Sheria amepata tuzo ngapi ndani na Nje ya Nchi lakini ambayo ameipata hivi karibuni ni ya Mbunifu Wa Mwaka Africa – 2017 katika tamasha la Abryanz Style & Fashion Awards ambazo hufanyika huko Uganda. Na alishindanishwa na wabunifu mbalimbali kutoka Nchi mbalimbali kutoka Africa  lakini alifanikiwa kuchukua yeye mbunifu kutoka Tanzania.

But then Sheria is No Avarage Guy, ana wavalisha ma – Rais kutoka Nchi mbalimbali za Africa na wabunge.

Tanzania needs to celebrate Sheria Ngowi, anafanya mambo makubwa na hajitangazi tu yeye bali ana tangaza Nchi nzima, anapo enda kuonyesha collection yake ya mavazi Nchi kama South Africa au London anaenda kama Sheria Ngowi mbunifu kutoka Tanzania, kama akifanya vizuri inamaanisha watataka kumjua na kujua Tanzania kunanini? ikiwa katika ulimwengu wa mitindo na vingine kwa ujumla.

 

 

Related posts

1 Comment

  1. rich89bet

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mbunifu-sheria-ngowi-ni-mfano-mzuri-wa-msemo-nabii-hakubaliki-kwao/ […]

Comments are closed.