Tukisema Tasnia ya mitindo Tanzania inakua hiki ndicho tunachomaanisha, zamani ilikuwa Mc anavaa tu hajali kuendana na sherehe lakini kwa sasa ma Mc wanajitahidi sana kama bwana harusi au bibi harusi akizubaa Mc anaweza kumfunika, Moja kati ya ma-Mc ambao wanafiwa na wanastahiki sifa katika mavazi yao ni Mc-Garab. Tumepata nafasi ya kuongea nae mawili matatu kuhusu style zake, pata kujua zaidi hapo chini
Afroswagga: fashion & style ina umuhimu kiasi gani katika kazi yako?
Mc garab: Fashion & Style ina nafasi kubwa sana as nasimama mbele ya watu ambao wananitazama na kunisikiliza at the same time. So inaongeza mvuto kwa audience yangu inafanya wasinichoke.
Afroswagga: Ulikuaje ukaamua kuwa the stylish mc as tunajua mc wengi huwa kawaida na mavazi
Mc Garab: Toka nimeajitambua kama kijana kipindi niko secondary nilikua na pendelea sana mambo ya fashion na style . Iko ndani yangu.
Afroswagga: Ni vipi huwa unachagua cha kuvaa katika sherehe as unaangalia uzito wa sherehe au?
Mc Garab: Uzito wa sherehe si saana dho ina nafasi yake kiasi flan , but kwa event kama Sendoff hua napendelea sana ku dress casual, Kia Afrika zaidi tofauti na Harusi ambapo mtoko unakua serious kidogo 😊.
Afroswagga: Huwa unaongea na wenye harusi kabla ya kujua uvae nini ili usiwazidi?
Mc Garab: Sure. Most of the time nawauliza ili kuepuka mfanano ambao pengine unaweza ukamficha bw harusi asijukikane yupi siunajua (Kidding) . But taarifa zinasaidiaga kidogo kulunguza over dressing na vitu kama hvyo.
Afroswagga: Tukiangalia mwili wako upo vyema je unafanya mazoezi? Mara ngapi kwa week?
Mc Garab: Tena nahisi nanenepa kwa kasi sana sikuiz. Ndo nataka nianze rasmi mazoezi sasa.
Afroswagga: Items 3 muhimu ambazo huwezi acha tembea nazo.
Mc Garab: My Phone comes 1st lol, Pafyum & body spray, duster ya viatu endapo nmepata kavumbi kidogo. You know 😉
Afroswagga: Favorite color, perfume/fragrance
Mc Garab: Navy Blue is bae, Calvin Klein ana taste nzuri sana,
Afroswagga: Ni accessories gani kuu every gentleman should own?
Mc Garab: Pocket Square kwa mvaa suit ni muhimu pale kwny koti wengi naona wanachukulia poa, Saa ya mkononi na ki Blacelet kidogo vinanogesha u gentleman.
Afroswagga: Tunaona unapenda kuvalishwa na wabunifu wa Tanzania, mbunifu yupi wa mavazi ya kiume kutoka Tanzania unapenda mavazi yake zaidi?
Mc Garab: Well kitu kimoja wengi hawajui mavazi yangu most of the time na mwambia fundi/ designer chakunitengenezea So naweza mpa mchoro au picha ( nibuni mavazi yangu) wao wanashona. So wote wangu coz hawaniangushagi.
Afroswagga: Maoni yako kwa wabunifu wa mavazi ya kiume Tanzania
Mc Garab: Bado sijaona Ubunifu ule konki ambao unanishtua kwa upande male cloth designers kwa apa Tz. Em waongeze ubunifu na kuacha ku copy copy kazi za watu wa nje.
Afroswagga: Awkward moment, ilishawahi kukutokea ukapendeza kuliko mwenye sherehe,ulikabiliana nalo vipi?
Mc Garab: Yes nakumbuka nlikua na This Six pieces Suit ikabidi nitoe koti nibaki na kizibao vinginevyo ningemnyong’onyesha mteja 🏃🏾
Afroswagga: Let’s play a game upo mbele suit inatatuka in an event. Utafanya nini cha kwanza?
Mc Garab: 🤣🤣 Ntapiga show nimekaa arif 🙌🏾🙌🏾 ButWhy 🙆🏽♂
Afroswagga: ulishawahi kuboronga kimavazi? Ilikuwaje?
Mc Garab: Yes. Nahisi najiamini sana . Confidence ilinibeba show ikaendelea.
Afroswagga: Does your wife influence your outfit ideas? Anakusaidia vipi kuchagua mavazi?
Mc Garab: Sure mara nyingi kabla sijafikiria cha kuvaa kwa ajili ya kazi ya siku husika nna hili swali maarufu kwake “ Navaa nini leo baby ?“ 😄.. Atanipa Ideas au nguo kabisa
Afroswagga: Your style icon?
Mc Garab; Nigerian EBUKA.. jamaa anajua
Afroswagga: Celeb gani unaona he has a good sense of style?
Mc Garab: Bongo Jux & Kiba , Mbele jamaa called Terrance Jay & David Beckham balaa.
Afroswagga: Chochote ungependa kuwaambia wa-Tanzania
Mc Garab: Sio kila fashion/style inayoingia ni yakushobokea wajue kuchuja pia wakizingatia unadhifu /kupendeza na maadili yetu kama wa Tz. 🥂
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you can find 25293 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mc-garab-akituambia-kuhusu-mitindo-na-style-zake/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 75028 more Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mc-garab-akituambia-kuhusu-mitindo-na-style-zake/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mc-garab-akituambia-kuhusu-mitindo-na-style-zake/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mc-garab-akituambia-kuhusu-mitindo-na-style-zake/ […]
sexophone jazz
sexophone jazz