SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mchanganyiko Wa Rangi Mzuri Utakao Nga’risha Vazi Lako
Mitindo

Mchanganyiko Wa Rangi Mzuri Utakao Nga’risha Vazi Lako 

Rangi ina nafasi kubwa sana kwenye maisha ya kila siku and the right ones zinaweza badilisha mood yako kabisa zaidi zikiwa ni rangi zinazowaka. So next time unataka kuweka mood yako sawa kwa kutumia mavazi basi mchanganyiko wa hizi rangi upo kwa ajili ya kazi hiyo. Ni rangi nzuri, zinazovutia na kuchamsha. Kama wewe si mvaaji wa rangi basi hili ni jaribio litakalokupa experience mpya na kukutoa kwenye comfort zone.

NYEKUNDU NA PINK

Can you believe it? Yani hizi rangi ni bonge moja ya combo. The pink inajua namna sahihi ya kufanya nyekundu ipop. Utapendeza bila kufanana na crown wala kachumbari hahaa. Usiongezee rangi sasa. Hata accessories zako hakikisha ni za rangi ya nguo au rangi kama nyeusi,dhahabu,silver au kijivu.

NJANO NA NYEUSI

Njano kama njano ni rangi inayong’aa sana tayari. Nyeusi sio rangi ya kung’aa sana lakini ikichanganywa na njano basi inawika sio kitoto. Alafu mtu mweusi na rangi ya njano ni kitu hatari, in short black and yellow ni the perfect match. So usiogope kuvaa ile nguo yako ya njano ambayo uwa unahisi haiendani na rangi nyingi.

BLUE NA KIJANI

Sitakuwa salad jamani? Hapana darling you won’t.. Ila tu usipoongezea accessories kibao zenye rangi mbalimbali. Viatu vyako vyenye rangi iliopoa na accessories kidogo and you are good to go. Blue na kijani ni magic kwa watu wenye uthubutu so jiamini and rock the look

ORANGE NA KIJIVU

Yes, i said. Njano na kijani…oop nimemaanish orange na kijivu. Sio combination unayoweza ifikiria kwa haraka kwakweli lakini ni mchanganyiko wa rangi unaopendeza kabisa. Ni juu yako tu kuamua vazi lipi liwe la orange na lipi la kijivu ila kwangu mimi naona kijivu inapendeza zaidi ikiwa kwenye vazi la chini

Imeandikwa na @style.with.mimie

Kama utajaribu moja ya rangi tulizo zitaja hapo juu usisite kututag kupitia account zetu katika mitandao ya kijamii

Related posts

2 Comments

  1. Carpet Cleaning Canal Winchester

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mchanganyiko-wa-rangi-mzuri-utakao-ngarisha-vazi-lako/ […]

  2. เปรียบเทียบประกันรถยนต์

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mchanganyiko-wa-rangi-mzuri-utakao-ngarisha-vazi-lako/ […]

Comments are closed.