SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Men Swim Wear Essentials
Mitindo

Men Swim Wear Essentials 

Linapokuja suala la kufurahia siku pembezoni mwa bahari au kuogelea, chagua vazi linalofaa la kuogelea na ni muhimu sana kwa starehe, mtindo pia kujiamini. Leo mavazi ya kuogelea ya wanaume yamebadilika zaidi na hii inampa option mwanaume kulingana na mapendeleo yake.
Tuchunguze chaguo bora zaidi za mavazi ya kuogelea kwa wanaume, tuanze na vipengele maalumu, mitindo na brands.


Classic swim trunks

Hizi ni shorts za urefu wa kati kwa kawaida huwa na kiuno laini na yenye matundu. Zinakuja kwa aina tofautu tofauti na rangi pia ili kuelezea mtindo wako binafsi, ukiongelea classic swim trunks huwezi kuacha kutaja brand maarufu kama speedo,quick silver na Ralph Lauren hutoa machaguo yenye ubora wa hali ya juu zinazochanganya mitindo mbalimbali.


Board Shorts

Ikiwa unapendelea urefu mrefu, basi aina hii ya shorts zitakufaa, hapo awali iliundwa kwaajili ya wasafiri, kaptula hizi za kuogelea kwa kawaida hufika chini ya magoti, Shorts hizi hufurahiwa zaidi na wale wanaopenda kuogelea maana huleta excellent mobility. Chaguo bora zinapatikana kwa brands kama Billabong, Hurley, O’neill ni miongoni mwa watoaji board shorts kali sana za wanaume.


Jammers

Ni kaptula ndefu za kuogelea zinazoenea kwenye goti au katikati ya paja, imeundwa kwa nyenzo zinazostahimili klorini. Jammers zinakupa conpressive fit with excellent shape retention. Brand kama Speedo, Arena, na Nike zinafahamika zaidi kwa utengenezaji wa kaptula hizi.


Swim-rash guards

Ikiwa unatafuta ulinzi dhidi ya jua basi aina hii ni chaguo sahihi, sio nzito na hukauka kwa urahisi sana na hutoa UPF ( Ultraviolet protection Factor) ili kulinda ngozi yako dhidi ya miale hatari ya UV, usiache kuchagua brand kama Quiksilver, Roxy na Patagonia hutoa ulinzi mbalimbali na maridadi na unaofanya kazi kukausha vipele vya kuogelea.


Usichukulie poa suala la kupendeza na kuchagua brands kali sio tu kwenye shughuli kubwa bali hata unapokuwa katika burudani kama kuogelea au unapotaka kupata upepo wa bahari, achana na suala la kuogelea na boxers its so old fashion, dear men just choose your style and rock it.

Imeandikwa Na @this_is_lydia

Related posts