Mei 20, 2022, mrembo Halima Kopwe alivikwa taji la kuwa Miss Tanzania, Halima amekuwa moja kati ya ma-miss wanao fanya vizuri kwakuwa tunamuona akishiriki events mbalimbali Nchini ziwe za kusaidia Nchi au majukwaa ya urembo, akiwa anajiandaa kwenda Miss World tumefanikiwa kufanya nae mahojiano kutuelezea amejiandaaje na tutegemee nini;
AFS: Well as Miss Tanzania 2022, toka uwe crowned hadi leo hii, waionaje experience nzima ya taji na crown hii ya Miss Tanzania? Malengo uliyoyapanga yameweza kutimia?
Halima: Being Miss Tanzania imekua ni experience tofauti sana kwangu, imenipa heshima, recognition na fursa nyingi sana lakini pia imenipa jukumu la kuwakilisha wasichana wa kitanzania duniani.. Tangu nimeshinda taji la miss Tanzania 2022 nimekua nikipokea compliments nyingi sana kutoka kwa mabinti wengi wakisema nawainspire kufuata ndoto zao kwasababu binafsi sikukata tamaa na ndoto zangu. Malengo yangu since the beginning yalikua ni kupeperusha bendera ya nchi yangu, I am so glad kwamba hilo ninaenda kulifanikisha for my own sake, for the country na pia kwa ajili ya wasichana wote wanaoniangalia kama kioo kwao.

AFS: Kila mlimwende wa Miss World lazima awe na project yake ya kijamii anayoisimamia that is being a BEAUTY WITH A PURPOSE,Waweza tuelezea project yako kiufupi, na kwanini ulichagua eneo hilo?
Halima: My Beauty with a purpose project inajihusisha zaidi na afya ya mama na mtoto kwa maana ya kuboresha afya zao na kuhakikisha tunapunguza idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi. The major inspiration ya hii project ilikua ni mmoja wa wanafamilia yangu, alipata bahati ya kuwa mjamzito lakini baada ya miezi nane alipoteza mtoto wake akiwa tumboni.. The whole experience ya yeye kupoteza mtoto wake kabla hata hajazaliwa ilinifunza kwamba maumivu ya kumpoteza mtu hayapimwi kwa umri maana hata kiumbe ambacho bado hakijaiona dunia pia kinaweza kuleta maumivu kwa familia nzima.. Niliamua kufanya mradi huu ili kusaidia situation kama hizi zisiwatokee watu wengine na pia kuunga juhudi za mh. Raisi Mama Samia Suluhu Hassan kwenye campaign aliyoianzisha ya #jiongezetuwavushesalama ambayo pia ina lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi..Nimeipa project yangu jina la *My Blood My Generation* , *Damu Yangu Kizazi Changu* kwani vifo vingi vinatokana na wajawazito kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua hivyo tunaweza kuwasaidia kwa kuhakikisha tunachangia damu mara kwa mara ili upatikanaji wa damu ya kuwaongezea wenye uhitaji unakua rahisi.

AFS: Watanzania na wadau mbalimbali wanaweza kuku-support vipi katika project yako?Pia kuna zoezi la upigaji kura, waweza tufafanulia mchakato unakuwaje na watanzania wanaweza kuparticipate vipi?
Halima: As for my project, mnaweza kunisupport kwa kuunga mkono juhudi zangu za kuhamasisha vijana na watanzania kwa ujumla kuchangia damu mara kwa mara, na pia kuchangia initiative yangu ya kugawa bima za afya kwa watoto ili kuhakikisha watoto wanapata msaada wa kiafya wanapouhitaji. Maelezo yote ya kunisaidia kwenye hii project yapo kwenye ukurasa wangu wa BWAP (beauty with a purpose project) @mgmb_movement ambayo nimeiweka kwenye instagram bio yangu.
Mshindi wa miss world multimedia, yaani mwenye kura nyingi zaidi kuliko wote anapata nafasi ya moja kwa moja kuingia kwenye robo fainali (semi-finals) za miss world na unaweza kunipigia kura mimi kwa kufata hatua hizi:
1.PAKUA APPLICATION YA MOBSTAR inayopatikana App Store na Playstore.
2.Fungua akaunti
3.Tafuta ukurasa wangu rasmi (MISSTANZANIA2022🇹🇿)
4.FOLLOW
5.LIKE Picha zangu zote.
Kumbuka LIKE MOJA NI SAWA NA KURA MOJA.

AFS: Hadi sasa ulipofikia, waionaje support toka kwa familia? Wadau wa urembo? Pia serikali na watanzania kwa ujumla?
Halima: So far nimekua nikipata support kubwa sana kutoka kwa familia yangu, marafiki na watanzania kwa ujumla. Sijawahi kupata kipingamizi chochote kwenye familia yangu na hata watanzania wengine ambao siwafahamu wamekua wakinisupport sana kwenye mitandao ya kijamii..
Nimefanya kazi pia na taasisi na wadau mbalimbali kama TAMA (Tanzania Midwives Association), Licks Pharmacy, Mpango wa Taifa wa damu salama, NHIF na CCBRT kwa namna tofauti tofauti katika muendelezo wa mradi kazi wangu.
Ningependa tu kuwaomba watanzania wenzangu wazidi kunipa support maana ushindi wangu mimi ni ushindi wa taifa zima.

AFS: Tungependa kuona ukiiwakilisha nchi ukiwa na mavazi ya wabunifu wetu toka nchini, je, umeweza pata ushirikiano katika hili toka kwa wabunifu nchini? Pia we are so excited kujua national costume, kuna any designer in Tz ambaye una-collaborate naye katika hili? Na any sneak pics and tips?
Halima: As of the moment bado niko kwenye maongezi na designers mbalimbali kama Rommy Jay tz ambaye alidesign costume yangu kwenye finals za miss tanzania, ila pia i’m trying to reach out kwa designers kama talented designer diana magesa cause I believe ana experience zaidi kwenye designs za international pageants.
Tukiachana na national costume design, miss world as a whole ni platform ya kuonyesha cultural heritage na uwezo designers wa nchi mbalimbali..
I have already recorded my introduction video to miss world ambayo nimeshirikiana na local designers kama Michael william’s na shantele designs and stylists like concious diddy, photographers like canny sophen and so much more.
Ningependa pia kuchukua nafasi hii kuwaomba wabunifu mbalimbali kuniunga mkono kwenye safari yangu ili niweze kuiwakilisha Tanzania kikamilifu kwenye jukwaa hili. Contestants wa miss world mara nyingi wanakaa kambini kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Huu ni muda tosha kabisa kuonyesha ubunifu wa tanzanian local designers so I call upon them ili tuweze kushirikiana kuionyesha dunia uwezo wetu.
AFS: As Miss Tanzania 2022, kipi kikubwa umejifunza kupitia taji hili ambacho waweza ishauri jamii na wasichana wenye ndoto za kushiriki mashindano ya urembo?
Halima: Kikubwa nimejifunza kwamba mashindano ya urembo yanaweza kuwa kama daraja kwa msichana kufikia malengo makubwa zaidi kwenye maisha yake.. urembo ni sanaa kama sanaa nyingine na ni fursa inayoweza kuwasaidia wasichana kupata riziki, hivyo kuwa na end goal ni muhimu sana kabla ya kushiriki. Ni lazma ujue unataka nini kwa mfano Mimi nipo zaidi katika kazi za kijamii na imenisaidia sana kupata support ya wadau mbalimbali kirahisi, kuna waliolitumia jukwaa hili katika modelling kama millen magese, kuna waliolitumia katika biashara kama mama Alaska, kwenye sanaa ya uigizaji na muziki kama feza kessy na wema seputu, wengine katika uongozi kama hoyce temu, bassila mwanukuzi na jokate.. Hivyo kuwa na end goal ni muhimu sana na kujua kuwa hii ni platform inayotupa kuonekana katika jamii. Hivyo, ni jukumu letu kulitumia vizuri ili kuijenga tasnia nzima na si kuibomoa.
AFS: Bado wengi katika jamii wanahisi urembo ni uhuni na familia nyjngi haziruhusu watoto wao wa kike kushiriki? Maoni na ushauri wako ni?
Halima: Kwenye maisha tunashauriwa siku zote kuangalia the positive side of things rather than the negative.. Ukiangalia tasnia ya urembo, utaona kwamba kuna mazuri mengi yatokanayo na tasnia hii. Kuna warembo kama Nancy Sumari ambaye aliweza kufika kwenye miss world top 6 na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia.. Kuna fursa nyingi sana zinazotokana na mashindano haya kama endorsements, patnership na makampuni makubwa na pia mashindano haya yanawakuza na kuwafunza warembo kujiamini na kujithamini.. Sifa hizi zimeweza kuwasaidia warembo kama mh. Jokate Mwegelo, Hoyce Temu , Basilla Mwanakuzi nk kushika nafasi mbalimbali za kiserikali. From this you can already see kwamba Urembo ni heshima, kama kauli mbiu ya the new miss tanzania inavyosema.
AFS: Tunakutakia kila la kheri katika kuiwakilisha nchi, uweze kuipeperusha bendera ya nchi yetu juu.
Halima: Asanteni sana.. nawaahidi i’ll do my best kuionyesha dunia mazuri na uwezo wa watanzania🇹🇿.. #Tanzaniatotheworld🇹🇿
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…