Tumezoea kuona wanawake pekee wakivaa vizuri na kupendeza katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Wanaume wachache sana wanao jua kupangilia mavazi yao wakapendeza katika Ramadhani. Wengi wao wamezoea kuvalia kanzu nyeupe au suruali kwa sababu zinavuka magoti mara nyingine hupendelea kuvaa kanzu kubwa kuzid miili yao, Kasumba ilyojengeka miongoni mwa lio wengi nikwamba mwanaume hatakiwi kupendeza, la hasha kila mtu ana pashwa kuwa na muonekano wa kuvutia awe mwanamke au mwanaume, mtoto au mtu mzima wote wanatakiwa kupendeza.
Tips chache za nini mwanaume avae ili aonekane wa kisasa na kupendeza katika kipindi hiki cha Ramadhani
KANZU ZA RANGI TOFAUTI NA ZINAZO KUTOSHA
Imezoeleka kanzu nyeupe pekee ndo ana takiwa kuvaa mwanaume. Siku hizi mitindo inakua ubunifu unaongezeka, zimebuniwa kanzu za rangi tofauti tofauti na zenye nakshi nzuri. Kwa mwanaume mweupe anaweza kuvaa kanzu nyeusi au ya rangi ya buluu iliyo kolea. Kwa mweusi anaweza kuvaa nyeupe au kijivu. Hakikisha ina kutosha na kuendana na mwili wako sio kwa sababu kanzu pana ukanunue hata ambayo haikutoshi haito pendeza. kanzu ikivaliwa na makobazi mazuri masafi ikiongezewa balagha shia na koti inayo endana na kanzu basi utapatikana muonekano mzuri kabisa.
KURTA (KANZU FUPI YENYE SURUALI YAKE)
Siku hizi zipo kanzu fupi zilizo na suruali yake kwa ndani ambazo pia zimebuniwa zipo za rangi tofauti tofauti, pia rangi tofauti tofauti inategemea na uhitaji wa muhusika na isiachie wala isibane sana, mara nyingi wanaume hupenda kuzivaa bila ya kofia lakini vyovyote vile zinapendeza
KIKOI/MSULI
Hivi huvaliwa hasa na wakina baba watu wazima na hasa wakiwa ufukweni, lakini pia vinaweza kuvaliwa mtaani na shati la mikono mirefu, makobazi na balaghashia.
Related posts
2 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mitindo-ya-kiume-katika-mwezi-mtukufu-wa-ramadhani/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 75158 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mitindo-ya-kiume-katika-mwezi-mtukufu-wa-ramadhani/ […]