SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mitindo Ya Unisex Inavyokuja Taratibu Nchini Tanzania
Mitindo

Mitindo Ya Unisex Inavyokuja Taratibu Nchini Tanzania 

Tuliwahi kuongelea kuhusu unisex fashion na namna ambavyo wabunifu wanavyo buni mavazi ya aina hii kwa kasi, Unisex  fashion and style ni mavazi yanayobuniwa na kuweza kuvaliwa na jinsia zote yaani ya wanaume na wanawake. Hii ni kwa mashati, sketi, suruali na hata accessories za mwilini.

Kwa sasa tunaona style hii ikiwa inaingia Tanzania taratibu, ikiwa ni wabunifu kubuni mavazi ya aina hii lakini pia tumeona watu maarufu mbali mbali wakiwa wanavalia mavazi na accessories za namna hii, kwa upande wa kike ilichukua muda kuona wanawake wakiwa wanavaa suruali Africa au hata hapa Nchini kwetu ilikuwa inaitwa uhuni, lakini taratibu ikakubalika na kwa sasa wanawake wanavaa suruali kama ambavyo wanauwe wanavaa bila kuwa judged.

Inaonekana shilingi inataka kugeukiwa kwa wanaume nao kuanza kuvaa mavazi na accessories ambazo zinaaminika za kike, tumeona watu maarufu mbalimbali wakiwa wamebeba mikoba ya kike, kuvaa vikuku lakini pia hata kubeba mikoba,kwa hapa kwetu Tanzania tumeona watu maarufu kama Diamond Platnumz akiwa amevalia kikuku, alipata backlash kubwa sana lakini ilionekana sio yeye tu Duniani ambae amevaa kikuku, watu kama Chris Brown na Dwayne Wade nao walishawahi kuvaa

 

Wakati tukiwa tunamuongelea Diamond, tukamuona mwanamitindo Calisah ambae yeye alikuwa kazini na akavaa viatu vya kike katika kutangaza duka hilo la viatu na alipo ulizwa alijibu kwa kusema kama akilipwa vizuri hata gauni anaweza kuvaa yupo kazini, na yeye pia alipokea backlash kubwa kutoka kwa watu mbalimbali lakini pia na yeye si mwanaume wa kwanza kuvaa heels Duniani watu maarufu mbali mbali na hata models wakiume kutoka Nchi za wenzetu huvaa viatu hivi, akiwepo mbunifu na Rapper Kanye West.

Wakati juzi tumemuona msanii anaye chipukia Twaha Mabantu, yeye aliamua kuvaa gauni kabisa amemalizia na viatu na socks,hii ikatufanya tu-notice kwamba kama ambavyo wanawake waliweza taratibu kuvaa mavazi ya kiume basi ndivyo ambavyo mtindo wa wanaume kuvaa mavazi ya kike na urembo wa kike unavyo anza kukua taratibu na inawezekana ikafika kipindi tukawa tunavaliana mavazi bila ya watu kushangaa wala kutoa backlash

Well afromates je mtaikubali hii style ya wanaume kuvaa mavazi ya kike kama ambavyo wanawake wanavaa mavazi ya kiume?

 

Related posts

2 Comments

  1. one up mushroom bar reviews

    … [Trackback]

    […] There you will find 22104 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mitindo-ya-unisex-inavyokuja-taratibu-nchini-tanzania-20669/ […]

  2. hawaiian magic mushrooms

    … [Trackback]

    […] Here you can find 77796 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mitindo-ya-unisex-inavyokuja-taratibu-nchini-tanzania-20669/ […]

Comments are closed.