Asante kwa muimbaji Jidenna kwa wimbo wake “Classic Man” sasa kila mwanaume ana hash tag, ni vizuri kwa wanaume nao kujisifia mara moja moja lakini sio tu ujisikie bali ina takiwa ufanye na vitendo pia kuwa “classic man” sio maneno tu bali una hitaji “confidence, clean na cut” hapo ina maanisha uwe una “Jiamini, Msafi na uwe na Minyoo ya nywele safi”.
Kujiamini (confidence) sio kwa kujisifia tu bali ni miondoko, jinsi unavyo ongea na kuweza kufanya kile unacho kiahidi, Usafi hapa ni muhimu mno wanaume wengi usafi wao wa nje ila una weza kukuta socks chafu, chumbani kwake kuchafu kuwa classic man ni kukamilika kila idara si tu chumba na mavazi bali hata tabia. na mwisho ni kunyoa hapa kila mwanaume ana takiwa kuwa na ndoa mbili (1) ni ya yeye na mkewe na ya (2) ni ya yeye na kinyozi, kuwa na yule kinyozi mmoja ambae ana kupatia kukunyoa na si kukunyoa tushaghala baghala.
Lakini pia U “classic man” una hitaji kuwekeza katika vitu viifuatayo
Viatu Vizuri – si tu kwa kuvutia bali vizuri visafi na viavyo dumu kwa mwanaume huitaji pea nyingi sana za viatu chache tu lakini hakikisha una sandals, raba, na “mshite” hivi ni vile vya kipapaa vikali, ukiwa na pea hizo chache zi weke safi na tuamini tunapo kwambia wanawake huwa wanaangalia viatu vya wanaume kabla ya kuchunguza kitu kingine chochote
lakini hii pia haimaanishi uvae viatu vizuri halafu uvae mavazi mabaya hapana unahitaji pia kuwekeza katika
Nguo – Hapa una hitaji nguo nzuri “tunapo sema nguo nzuri tuna maanisha nguo nzuri” na sio nguo za bei ghali, una weza kununua nguo ya bei ghali na isiwe nzuri, tafuta nguo nzuri ambazo zinaendana na mwili wako kuwa na mashati ya vifungo mazuri, suruali za jeans, suti, kaptura na t – shirt hii ina kusaidia kubadilika kutokana na muda huwezi kwenda beach na suti.
Urembo – ndio urembo hata wanaume wana takiwa kuwa nao, urembo kama saa, kofia, miwani na tai pia hata vikoti vya hapa na pale na pia usisahau kuhusu rangi, wanaume wengi huwa wana amua kuchagua rangi fulani labda nyeusi, nyeupe, brown na blue wakiogopa kuvaa rangi za kuwaka kama kijani, nyekundu n.k kuvaa hizi rangi haimaanishi wewe ni mwanamke jaribu tu ku matchisha na uta pendeza mno.
Related posts
3 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mjue-classic-man/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mjue-classic-man/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mjue-classic-man/ […]