SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Muonekano Mpya Wa Duka La Mbunifu Ally Remtullah
Mitindo

Muonekano Mpya Wa Duka La Mbunifu Ally Remtullah 

Jumamosi hii tuliweza hudhuria ufunguzi wa Ally Rehmtullah’s store baada ya matengenezo makubwa. Toka mwaka jana tuliweza ona kipupgrade baada ya kuingia katika partnership na Flygle NA Hightech wear.

Katika ufunguzi huu nani ni nani wa tasnia ya ubunifu na mitindo walijumuika kuungana na Ally wakiwemo wabunifu, models, photographers, bloggers na media houses. Nasi Afroswagga tulikuwepo kuweza kijionea ufunguzi huo ambao uliambatana na wabunifu wengine wakipewa nafasi kuonyesha baadhi ya kazi zao.

Ally Rehmtullah alifafanua kuwa katika kutoa nafasi kwa wabunifu wachanga, kila baada ya miezi mitatu, wabunifu wachanga watapewa nafasi ya kuonyesha baadhi ya kazi zao katika store yake. 

Baadhi ya wabunifu na brands zilizoweza onyesha na kuuza kazi zao siku hiyo ni Kiki’s Fashion, W Style Loft, Shahbaaz Sayed, Mgece Cici Designs pamoja na #TheStreetsOfDSM toka kwa Ngaira Mandara.

Pia tulivutiwa sana na Ngaira Mandara mwenye brand ya The Streets of DSM. Ni kijana aliyeweza kuibuni Dar es Salaam na kuiweka katika Sanaa. Kila kazi yak yaonyesha wana Dar es Salaam na maeneo yake katoka angle ya kipekee. Ana bidhaa mbalimbali zikiwemo t-shirts, vikombe, laptop bags na vingine vingi.

Pongezi nyingi kwake Ally Rehmtullah na twategemea kuona kazi nzuri Zaidi baada ya matengenezo na ufunguzi huu mkubwa.

Imeandikwa na @willibard_Jr

Related posts