SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Must Have accessories For Men
Mitindo

Must Have accessories For Men 

Wanaume wengi hawajui essential accessories kwa ajili ya mionekano na hawafahamu kuwa accessories husaidia kuinua muonekano wao katika siku husika kwa kukamilisha outfit yako.
Essential accessories for men
Wengi wanajiuliza zipi ni essential accessories kwao ambazo haupaswi kukosa kuwa nazo katika kabati lao. Zifuatazo ni essential accessories kwa wanaume **

1.watches
Ni dhambi kubwa kwa mwanaume kukosa saa mkononi mwake kwa sababu saa inatakufanya usionekane too plane yani uboe. Unaweza ukawa na saa za aina tofauti tofauti ambazo unahitaji wewe kulingana na siku husika ila usisahau saa katika outfits zako.

2.Bracelet
Ni aina ya essential accessory kwa wanaume ambayo haupaswi kukosa. Aina hii ya accessory unaweza kuvalia na outfits yoyote kwa sababu inakupa attention mikononi. Kwa sasa watu wengi wanapenda kuvaa bracelet upande ambao wamevalia saa yani mkono wa kushoto na pia unaweza kuvalia upande ambao haujavalia saa.

3.keyholder
Miaka imebadilika na siku zinaenda accessories kwa wanaume zinabadilika siku baada ya siku utajiulizaje kwanini keyholders ziwe accessory, ukiwa na holder nzuri ambayo umeninginiza kwenye suruali yako inaweza kusaidia sana kukupa attention na kukufanya uonekane mwanaume ambae una own vitu fulani hivi makini hauwezi ukawa na keyholder halafu usiwe na vitu una own hata kama ni vidogo.

3.chain
katika moja ya accessories ambazo unatakiwa uwe makini nazo ni chain unatakiwa uwe na chain ambayo inaendana na style yako usiwe na chain ambayo hauwezi kuvaa kama wewe ni mtu wa casual basi usivae chain ambayo ina mambo mengi cha muhimu unatakiwa uwe na chain ambayo utaweza kuvaa na itakufanya muonekano wako uwe perfect.

4.Belt
Ninaposema mkanda sio bora mkanda tu unatakiwa uwe na mkanda ambao ukionekana utamvutia mtu anayeangalia yani uwe na mkanda mzuri ambao utaongeza muonekano wako kama ukiamua kuchomekea. Kuna aina nyingi sana ya mikanda ila inabidi uchague mkanda ambao utakufit na muonekano wako na aina ya outfit ambayo unayovaa siku husika na vazi husika please usisahau kuvaa mkanda ambao utaupenda wewe kwanza then ndo umvutie mtu mwingine.

5.Glasses
miwani kama miwani ni muhimu sana kama utavaa aina ya miwani ambayo itaendena na outfit zako na hali ya hewa ya sehemu husika. Jitaidi sana uvae miwani ambayo itaendana na shape ya sura yako.

6.Cap
Hii ni aina ya accessory ambayo inaweza ikakupandishia muonekano wako kwa asilimia kubwa sana unaweza kuvaa cap weekend ukitoka na marafiki na itakufanya uwe na comfortable kwa sababu kuna siku utatamani kuficha nywele zako kwa sababu tofauti tofauti na still itakufanya uonekane stylish.

7.Tie and scarf
Unaweza ukadhani ni vitu vya kawaida sana ila tie na scarf kwa mwanaume sio vitu vya kukosa ukiwa navyo itakusaidia sana kuboresha muonekano endapo utavaa scarf au ukavaa tie na shirt na bado ukatokelezea kijanja sana.

8.Purse and briefcase
Ukiwa mwanaume wa style ya casual basi hautakiwi kukosa purse na hata briefcase kwa sababu itasaidia kukuongezea attention kwa audience ambayo inakuzunguka. Purse na briefcase inasaidia sana kuhifadhi baadhi ya vitu ambavyo ungeshika mkononi ingekufanya muonekano wako uonekane haujakamilika na kukufanya uonekane mwanaume ambae haujitambui.

9.Ring
Pete kama pete ukiwa umeoa basi fanya pete yako iwe accessory na hata kama haujaoa basi vaa pete ambayo itafanya muonekano wako uwe mzuri usivae pete tu ambayo mtu akikuona nayo ashindwe hata kukuuliza hiyo pete umenunua shingapi.

NOTE : kunukia vizuri napo ni essential accessory, hautakiwi kukosa kunukia vizuri jitahidi unukie vizuri mda wote si unajua wanawake wanapenda mwanaume anayenukia vizuri yani “Nothing is more memorable than a good smell”

imeandikwa na @gotchathegreatest

Related posts