Kama wewe ni moja kati ya wafuasi wa Mwasiti hili na wewe utakuwa umeliona, Mwasiti ni moja kati ya wasinii wenye vipaji vikubwa kabisa katika sekta ya muziki, ni kama Lady Jay Dee wa miaka hii. Ukiachana na wengine ambao huwa wanasingizia miili yao kwa kutokupendeza Mwasiti ni moja kati ya wanadada walio jaaliwa umbo zuri kabisa ambalo wengi wanalilia.
Waswahili husema upele umpata asie na kucha basi hili neno linam-fit kabisa Mwasiti, wakati wakina Shilole wanaenda gym kukonda ili wapate kupendeza na kuonekana vizuri katika mavazi, Mwasiti yeye anamwili na wala hajisumbui kuhusu mavazi. Ukikutana au ukiona picha ya Mwasiti katika mitandao huwezi kupata ile wow look ni kwamba yupo ordinary kama sisi wengine
Inawezekana anapenda kuwa simple lakini haimaanishi ndio uwe simple kupitiliza kiasi ambacho uwe sawa na sisi ambao hatujulikani, kama kuna factor kubwa katika kuwa mtu maarufu hasa mwanamuziki, mwanamitindo, muigizaji basi ni muonekano wako, kile ambacho unakionyesha katika jamii ndio ambacho kitawavutia wengi zaid, ukimuona mwasiti huwezi kuamini yeye ndio alii-hit na nyimbo kama hao,Nalivua pendo nk.
Tungependa kumuona Mwasiti akiwa katika mionekano tofauti mizuri, ukizingatia ana mwili ambao anaweza kuvaa chochote kikakaa, well sio lazima vi-crop top au mini skirt lakini tudanganye basi hata na vigauni na outfit zinazoeleweka. Na wala sio kuhusu hela bali ni kuelewa nini unataka na kuamua kuamka na kuji-style, katika wasanii 10 ambao wako ordinary Mwasiti yupo katika top 3.
Ukiingia katika page ya Mwasiti Instagram ukikutana na picha nzuri amependeza basi ni cover ya wimbo wake mpya, na nyingi zinajirudia, Mwasiti kupendeza si tu kwenye nyimbo unahitaji kupendeza hata katika maisha ya kawaida tusiende mbali kwa stylist bali ni wewe kujifunza kuvaa mavazi na ukaeleweka kutokana na status yake katika jamii. Well shade yetu ya leo imemuangukia Mwasiti je unadhani nani mwingine ana paswa kupewe ukweli wake? tuandikie hapa.
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwasiti-almas-ana-kwama-wapi/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 25956 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwasiti-almas-ana-kwama-wapi/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwasiti-almas-ana-kwama-wapi/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwasiti-almas-ana-kwama-wapi/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwasiti-almas-ana-kwama-wapi/ […]