Birthday mama Naseeb Abdul A.K.A Diamond Platnumz ni week ijayo na by the look of it theme ni ya birthday hio itakuwa ni The Great Gatsby.Tukianza na The Great Gatsby ni nini, hii ni novel iliyoandikwa na muandishi kutoka America aitwae F. Scott Fitzgerald , Novel hii inahusiana na Billionaire aitwaye Jay Gatsby ambae alikuwa na passion na obsession na binti aitwae Daisy Buchanan. Novel iliandikwa mwaka 1922 na kuwa published mwaka 1925.
Baada ya kujua kidogo kuhusu historia ya novel hii tujue kiundani kuhusu theme ya mitindo hii, kama ambavyo tumeona novel imeandikwa miaka ya 20,inamaanisha tunaongelea kuhusu kipindi hiko watu walikuwa wakivaa nini.

Hii ni miaka ya katikati kati ya World war I & II, kwa inavyosemekana miaka hii watu walikuwa waki party like never before na wanawake walikuwa huru ku-explore mitindo, ni miaka ambayo wanawake walianza kuvaa nguo za kiume, kuvuta sigara, kukata nywele fupi na kwenda kwenye sherehe bila kusindikizwa.
With that being said tuone walikuwa wakivaa nini?
Wanawake walikuwa wakivaa Flappers, hizi ni gauni fupi na ziko loose kidogo (hazibani), hazina mikono na mara nyingi walikuwa wakizivaa na gloves. Gauni hizi hupambwa na lace, sequins, cutaways, patterns au tassels , mfano mzuri ni kwenye picha hapo chini


The Evening Dress
Miaka ya 20’s fashion ilikuwa lose ( nguo ambazo hazibani sana), Kwa evening dress wanawake walikuwa wakivaa magauni marefu ambayo hayana mikono na ball gowns, mara nyingi zilikuwa za velvets na silks zikiwa na dropped waistlines, sequins, appliqué na pleats. Rangi zilikuwa sio za ku-shout

Wanawake pia walikuwa wakivaa nguo za kiume, hasa suit mfano mzuri wa evening dress na wanawake kuvaa nguo za kiume ni hio picha hapo chini ya Kylie Jenner na dada yake Kourtney Kardashian.

Kwa viatu wanawake walikuwa wakivaa block heels, wanaume ni Brogues shoes, lakini pia kichwani walikuwa wana accessories zao ambazo walikuwa wakivaa kama turban au head wraps,pearl clutch, statement necklaces, rhinestone earrings na gloves. kwa wanawake huku wanaume wakivaa mzee ojwang hats.



Makeup – walikuwa wanapenda bold lipstick hasa nyekundu, unaweza kupaka rangi yoyote uiependayo na inayoenda na vazi lako, hair styles za miaka hio ni short hair au deep finger wave hair style.

kwa wale wapenda ki- Africa zaidi unaweza kuwa inspired na hizi picha hapa chini


Photo credit – jamilakyari.com designer – keemharun
Ni matumaini yetu tumekusaidia kuelewa theme kwa namna moja au nyingine lakini kama bado unaweza kuangalia movie inayoitwa The Great Gatsby itakusaidia zaidi.
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwongozo-wa-namna-ya-kuvaa-great-gatsby-style-katika-birthday-ya-mama-diamond/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwongozo-wa-namna-ya-kuvaa-great-gatsby-style-katika-birthday-ya-mama-diamond/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwongozo-wa-namna-ya-kuvaa-great-gatsby-style-katika-birthday-ya-mama-diamond/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwongozo-wa-namna-ya-kuvaa-great-gatsby-style-katika-birthday-ya-mama-diamond/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/mwongozo-wa-namna-ya-kuvaa-great-gatsby-style-katika-birthday-ya-mama-diamond/ […]