SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna 3 Za Ku-Style Cargo Pants
Mitindo

Namna 3 Za Ku-Style Cargo Pants 

Kama tunavyojua Y2K fashion imerudi, style nyingi ambazo zilikuwa zinatumika miaka ya zamani zinaonekana kurudi kwa kasi na kwasasa kubwa tunayoiona ni cargo pants. Kama hujui Cargo Pants ni nini ni zile suruali ambazo zinakuwa na mamifuko makubwa na mara nyingi huwa zinakitambaa kigumu japo kwasasa zimetoka za material mbalimbali.

Inawezekana unayo na hujui ui-style vipi au unajua na namna ya kui-style ila ungependa kupata namna nyingine nyingi za ku-style vazi hili basi tupo hapa kwaajili yako.

Na Tshirt / Top

Inategemea na uendapo na mapenzi yako kama huna mtoko wa maana unaweza kuvaa na simple sandals au kicks lakini kama una mtoko basi unaweza kuvalia suruali hizi na heels kama Kim Kardashian hapo chini

Cargo Pants Na Crop top

kuna wale tunapenda kuonyesha matumbo au kuwa stylish kwa kuvaa crop top unaweza ku-style cargo pant yako na crop top, unaweza kuongezea na jacket juu au hivi hivi na kupendeza.

Cargo Pant Na Body Suit

Cargo pant inaweza kuvaka na body suit, uka istyle kutokana na mazingira uliyopo au unayokwenda, unaweza kuvaa off shoulder bodysuit, spaghetti strap body suit au hata body suit ya mikono mirefu ni wewe na comfortability yako.

Cargo pants zinaweza kuvaliwa na chochote iwe kuanzia shirts, vest’s, corset top’s na nyinginezo lakini pia zinaweza kuvaliwa na boots ziwe ndefu au fupi, raba, heels etc. Na unaweza kuvaa kwenye mitoko ya usiku, date, casual wear na hata kwenda brunch na marafiki. Well hizi ni chache ambazo tumeweka lakini zipo namna nyingi nyinginezo unazoweza ku-style vazi hili, muhimu ni kujua namna ya kucheza nalo.

Related posts