SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna 5 Za Kuonekana Stylish Kazini
Mitindo

Namna 5 Za Kuonekana Stylish Kazini 

Moja kati ya vitu ambavyo wengi tunapitia ma-ofisini ni kuwa confused kati ya kuwa over dress na ku-low dress ofisini na chaguo kubwa huwa kuwa katikati yaani usiwe low wala over dressed na hapa ndipo tunapokutana wengi unakuwa na ma shirt yako ya rangi moja kadhaa, skirt kadhaa na suruali ukamalizia na handbag yako na viatu basi mwisho wa siku ofisi nzima tunafanana kasoro rangi za nguo tu lakini ni namna gani unaweza kuwa stylish ofisini?

Toka Kwenye Plain Clothes Na Anza Kuvaa Pattern

Wengi ofisini tunavaa plain clothes utakuta umevaa plain white shirt na plain black trouser au skirt, toka hapo na anza kuvaa zenye pattern kama top plain basi chini valia suruali/skirt ya pattern na kama skirt / suruali plain valia top yenye pattern hakikisha rangi zinaendana

Vaa Mavazi Ya Rangi

Hakuna sehemu imeandikwa rangi za mavazi ya kazini yawe black, white, au blue tu jamani kuna colors nyingi ambazo zina pop lakini zimetulia vyema tu unaweza kuvaa ofisini kama maroon, emerald green, mustard yellow etc lakini pia hakikisha hazipigi kelele sana na kama utavaa juu rangi ina pop chini vaa calm color

Pop Color Na Viatu / Handbag

Kama sio mpenzi wa mavazi ya rangi rangi basi kati ya viatu au handbag hakikisha ina rangi ya kuvutia ambayo itafanya wengine wageuze shingo kukuangalia wewe

Accessorize

Miwani sio mpaka uwe unaumwa macho jamaniunaweza kuvaa tu kama accessory kuna miwani ambayo ni kama ya macho lakini ni ya urembo unaweza kuchagua unayoona inakufaa ukavaa, vaa belt pale vazi lako ninapohitaji mfano unavaa black little dress unaweza kuongezea na animal print waist belt, pochi pia inaweza kuwa namna nzuri ya kuongezea udambwi kwenye vazi lako la ofisini

Well Tukutakie Slayage Njema Week Hii

Related posts

2 Comments

  1. tiktok download video

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-5-za-kuonekana-stylish-kazini/ […]

  2. 토렌트 다운

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-5-za-kuonekana-stylish-kazini/ […]

Comments are closed.