SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna 7 Za Kipekee Za Kustyle T shirt
Mitindo

Namna 7 Za Kipekee Za Kustyle T shirt 

Kuna nguo zinaendana na kila kitu. Yani hizi nguo ukinunua ni kama vile umewekeza..hautajuta. Kwanzia kwenye good days hadi zile siku hutaki kusikia suala la kuvaa, basi hizi nguo uwa tayari kuvaliwa. Tshirt ni miongoni mwa hizi nguo. Unaweza kuvaa tshirt na kitu chochote hususani ikiwa plain lakini ni namna gani unaweza ivaa ukatokea kipekee zaidi? Niko hapa kukueleza namna unaweza style tshirt yako kama ifuatavyo. Usisahau style ni uhuru kuwa uhuru kufanya majaribio na nguo zako unaweza pata muonekano nadhifu zaidi.

Imeandikwa na @style.with.mimie

T Shirt , sketi na raba

Huu muonekane uwa casula ila ni casual kali hatari. Unaweza vaa sketi ndefu inayobana, sketi fupi au inayofika chini kidogo ya magoti. Ni vizuri zaidi ukichomekea au ukiifunga shati kwa mbele kama umevaa sketi ya high waist au unataka tu kuachia ngozi kidogo. Aina ya viatu unavyovaa vinakamilisha muonekano. Unaweza kuongezea accessories simple ili kutunza muonekane wako, too many accessories zinaweza haribu the whole look.

 

 

 

 

 

 

 

Shati, jeans na kiatu kirefu

Wale wanaopenda smart casual looks, hii ni yenu. Kuna jeans za kila aina; sketi, suruali, pensi, mini skirt, overrall, yani kila aina. Imagine umetupia shati plain na zile suruali ambazo chini zimechanwa, kiatu kirefu na handbag kali. Umeona hatari inayotokea hapo? So muhimu ni kiatu kizuri. Unaweza vaa mkanda pia ili kuongeza vionjo.

 

 

 

 

 

 

 

Shati,koti na kofia

Ni muhimu kutoka kitofauti, watu wengi hawajazoea kuvaa kofia na koti ila this is a look. Unapoongeza accessories keep it simple na kama unavaa statement piece basi jitahidi iwe moja tu. Hakikisha unapangilia rangi zako vizuri na koti lako liwe zuri linaloendana na mavazi yako mengine na liwe linaendana na mwili wako.

 

 

 

 

 

 

 

 

Shati na kofia ya duara

Watu wachache wana ujasiri wa kuvaa hizi kofia, nataka na wewe uwe miongoni mwa hawa watu. Ukiwa na nguo yako iwe ni suruali, sketi, kaptula..n.k basi unaweza ivaa na shati na kofia ya duara. Shati unaweza kuifunga au unaweza chomekea. Unaweza vaa na high heels zilizo wazi, buti, flats au raba.

 

 

 

 

 

 

 

 

Shati kubwa na mkanda mnene au kiatu matata

Huu ni muonekano wa tofauti na unafaa zaidi mitoko na washkaji, sehemu za starehe na sehemu zote ambazo kuvaa nguo fupi sana sio ishu. So kama una shati lako, ni kubwa sana..unaweza livaa na boots zinaweza kuwa ni ankle boots au buti ndefu hadi magotin. Pia unaweza vaa na raba au kiatu kirefu chochotei. Bana shati kwa mkanda mnene au kufunga sweta kiunoni. Unaweza vaa na kofia au kuweka cheni. Cheza na mavazi yako.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Shati na kitenge

Kitenge ni vazi flani lenye rangi nyingi, ukivaa na shati plain basi unabalance mambo. Unaweza vaa na nguo yoyote ya chini ya kitenge na kunogesha muonekano kwa accessories mbalimbali. Hakikisha viatu vinaendana na muonekano wote.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Shati na suti

Kama unataka kupunguza makali ya suti a.k.a “tone down” basi vaa tshirt ndani ya suti. Hii itasaidia suti ionekane casual zaidi. Ukitaka kuwa casual zaidi basi ongeza na raba miguuni na vaa accessories chache sana, ikibidi usivae. Pia usivae rangi nyingi sana. Jaribu kumechi rangi ya shati na viatu au shati na mkoba.

Related posts

4 Comments

 1. เป็นหนองใน

  … [Trackback]

  […] There you will find 89580 more Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-7-za-kipekee-za-kustyle-t-shirt/ […]

 2. buy magic mushrooms in usa​

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-7-za-kipekee-za-kustyle-t-shirt/ […]

 3. ซื้อหวยออนไลน์

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-7-za-kipekee-za-kustyle-t-shirt/ […]

 4. buy ayahuasca tea online australia,

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-7-za-kipekee-za-kustyle-t-shirt/ […]

Comments are closed.