Moja kati ya watu ambao Nchi za wenzetu wanawatumia katika kuleta ushawishi wa mitindo kwenye jamii ni media personalities, kwa kusema media personality hapa tunamaanisha wale watu maarufu katika media yaani watangazaji, wale ambao wamepata umaarufu kupitia kitu fulani wamefanya kama washindi wa michezo fulani mfano Idris Sultan aliyepata umaarufu kupitia ushindi wake Big Brother, wale watu maarufu katika mitandao ya kijamii n.k.
Hawa watu wanaushawishi mkubwa katika jamii na mbele ya kamera za media mbalimbali. Ushawishi wao unawakusanyia watu wengi ambao wanawaangalia, endapo media personality akivaa vazi aina fulani au mbunifu fulani basi utaona wale wafuasi wake nao wakijaribu kuvaa kama yeye, na hii inaonekana sasa hivi ukipita kwenye mitandao ya kijamii, wauza urembo au mavazi wengi wanaunganisha picha ya msanii au mtu fulani anaefahamika akiwa amevaa hilo vazi na mavazi wanayouza wao. Ukiuuliza wafanya biashara hawa watakwambia mtu yoyote maarufu akivaa, kusuka au kutumia urembo unaouuza basi hivyo vitu huisha kwa kununuliwa haraka zaidi.
Kutokana na kwamba jamii inawaangalia endapo watachukua muda wao mfupi katika kuvaa au kuongelea kuhusu fashion, basi hii itawapa elimu jamii inayo wazunguka kuhusu namna gani na wao wanaweza kuwa fashionable, mfano mzuri Nchini Kenya host’s wa Television Loulou Hassan mara kwa mara huchukua muda wake kuwaelimisha wafuasi wake kwa namna wanavyoweza kufunga viremba vile ambavyo yeye hufunga.
Lakini pia wanaweza kutumiwa na wabunifu katika kutangaza kazi zao, si watu wote wanaojua mbunifu fulani anabuni au ana collection fulani ya mavazi, ukitumia kumvalisha media personality akasema amevalishwa na fulani basi hii taarifa inaweza kuwafikia wafuasi wake kwa urahisi na wao kujua kwamba vazi hili alilolivaa fulani limebuniwa na mbunifu fulani, mfano mzuri ni mtangazaji Amina Abdi Rabar kutoka Kenya, wabunifu wengi na maduka mbalimbali humvalisha Amina mara kwa mara na yeye anawatangazia kazi zao.
Vyombo vya mitandao vya kijamii vimefanya iwe rahisi kwa watu kuangalia watu wanaowapenda wamevaa na nini kipo kwenye trend. Kuna watu ambao huvaa vazi sababu tu fulani amevaa mfano kiatu akivaa Shadee au Bdozen basi na yeye angependa kuwa nacho, watu maarufu na ambao sio maarufu wanakitu kimoja kinacho waunganisha na hicho ni kwamba wote wangependa kupendeza, na kuonekana wanaenda kwa wakati kwa kuvaa trend zilizopo.
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ambavyo-media-personalities-wanaweza-kuleta-ushawishi-katika-mitindo/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ambavyo-media-personalities-wanaweza-kuleta-ushawishi-katika-mitindo/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ambavyo-media-personalities-wanaweza-kuleta-ushawishi-katika-mitindo/ […]