SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ambavyo Unavaa Ndivyo Ambavyo Unajisikia Kuhusu Wewe
Mitindo

Namna Ambavyo Unavaa Ndivyo Ambavyo Unajisikia Kuhusu Wewe 

Tumekuwa tukipata maswali mara mengi na wengine wamekuwa wakiwauliza fashionista’s na stylist vipi wanaweza kuwa wanaonekana vizuri siku zote? ukiachana na kwamba styling is an art lakini namna ambavyo unavaa mavazi yako au unajivalisha inatokana na jinsi unavyo jisikia kuhusu wewe.

 

Unaweza ukawa sio stylist lakini ukawa unajipenda mwenyewe na kupenda kupendeza, well hii inakuaje? unaweza kukutana na watu wa aina mbalimbali katika mazingira tunayoishi unaweza kukuta watu wanafanya biashara moja na inawezekana wakawa wanapata kipato kimoja lakini mwingine anapendeza sana na mwingine yupo tu kawaida, hii inaonyesha kuna yule ambae anajijali na kuna yule ambae ana attitude ya kutokujali.

Kama unaamini katika kujipenda mwenyewe basi ni dhahiri utajipenda ndani na nje, utapenda kuonekana umependeza na sio kwa ajili ya mtu ila unapata ile feeling ya satisfactions kwa kujipenda mwenyewe, tunaweza kusema looking good inaanzia deep down inside, je unajichukuliaje? unaself love? self confidence?

 

Mazingira tunayoishi yanachangia sana hapa utakuta wakati watoto wanakuzwa mmoja anasifiwa mzuri mwingine akiwa anaambiwa yah wewe mzuri lakini sio kama fulani, hii inamfanya mtoto kutokuwa na confidence ndani yake na anaweza kujichukia, mavazi yake yanaweza kuwa hideous ana jificha sio mtu wa kuvaa mavazi akajiachia na hii kwa sababu anahisi labda nikivaa mavazi ya kujionyesha itakuwa rahisi mtu ku-notice mimi si mzuri, lakini yule ambae anaambiwa ni mzuri always anakuwa anajiachia, well acha tukwambie kitu kila mmoja wetu anauzuri wake na unaanza na kujiamini mwenyewe hata sikumoja dont let one’s opinion kukufanya uishi maisha ambayo sio yako (kumbuka tunaishi mara moja tu make that moment worthy your stay) ishi watu wakiwa wanakukumbuka waseme aliishi maisha yake. Love Your Self & Slay The Entire Universe

Style inaingiliana na attitude, confidence & self love, It Is Not Just The Cloth But It Is Who You Are Internally

 

Related posts