SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ambavyo Watu Maarufu Wame-Style Kanzu Zao
Mitindo

Namna Ambavyo Watu Maarufu Wame-Style Kanzu Zao 

Tumeingia kumi la pili katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, Week iliyopita tuliona jinsi ambavyo watu maarufu mbalimbali wali-style mavazi yao wakati wamekwenda kufturu pamoja na kuzindua kipindi cha nyumba ya Imani katika wasafi headquater,

Well week hii tunaangalia watu maarufu mbalimbali walivyo style vazi la kanzu

Tuaze na Bdozen mtangazaji kutoka Clouds Fm, yeye alivalia Kanzu nyeupe, ameistyle na eghal ya rangi nyekundu na nyeupe amemalizia muonekano wake na miwani na kobazi na socks, he looks dapper as he always does.

Tunakuja kwa mwanamuziki Fid Q au Fareed Kubanda yeye aliamua kuvaa kanzu ya rangi ya blue ( ni mara chache kuona mtu amevaa kanzu ya rangi rangi), Kanzu hii ina urembo mweupe amemalizia muonekano wake na suruali nyeupe, eghal yenye rangi nyeusi na nyeupe na viatu vyenye rangi iliyo endana na kanzu. Fid looks good hapa unaweza kuona amefanya effort katika hili vazi, but well Fid fanyia utaratibu hizo ndevu basi hata kitana tu kipite all in all amependeza.

Gabo yeye ni kama ameupania hivi huu mwezi maana kila post amependeza hadi kazi kuchagua ipi tumeipenda zaidi ya ipi, leo tuna share nanyi outfit zake mbili kati ya nyingi alizopost ya kwanza hii ambayo aliamua kuvaa all white, kanzu nyeupe, eghal nyeupe, viatu vyeupe amemalizia muonekano wake na miwani, saa na kifimbo you can never go wrong in white.

 

Hapa ilikuwa same outfit sema akaongezea na hili dish-dash kwa nje, unaweza kuona jinsi ambavyo unaweza kuvaa vazi hili mara nyingi kwa kuongeza tu accessories mbalimbali.

Wa mwisho kwa leo tunamalizia na msanii Ommy Dimpoz ambaye na yeye alivaa all white kanzu nyeupe na turban nyeupe, amemalizia muonekano wake na miwani pia.

Well kama ambavyo unaona vilivyo inekana kuwa in common ni viremba, miwani na saa, kama ungependa kuvaa kanzu yako ionekane stylish basi ongezea hivyo vitu. Tuambie kwa upande wako nani kakuvutia zaidi kati ya hawa wanne?

 

Related posts

4 Comments

  1. w.ytmp3.bz

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ambavyo-watu-maarufu-wame-style-kanzu-zao/ […]

  2. ЗАРАБОТОК КРИПТОВАЛЮТ

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ambavyo-watu-maarufu-wame-style-kanzu-zao/ […]

  3. visit homepage

    … [Trackback]

    […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ambavyo-watu-maarufu-wame-style-kanzu-zao/ […]

  4. buy mushrooms portland​

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ambavyo-watu-maarufu-wame-style-kanzu-zao/ […]

Comments are closed.