SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kuonekana Stylish Ukiwa Umevalia Suit
Mitindo

Namna Ya Kuonekana Stylish Ukiwa Umevalia Suit 

Suit ni moja ya vazi ambalo lima heshimika sana,na mara nyingi huwa lina kuwa styled simple maana tayari lenyewe linaongea. Lakini sometimes kuwa simple sana kunaweza kufanya muonekano wako uonekane basic, kama wewe ni moja kati ya wale ambao wanavaa suit kazini au kwenye mikutano na sehemu mbalimbali na ungependa kuonekana more stylish basi hizi tips chache zitakusaidia,

  • Rangi

Wengi wetu huwa tuna zile suit ambazo zinarangi za kutulia mfano blue, nude, black etc lakini pia unaweza kuwa tofauti kwa kuchagua rangi ambazo ni bold, mfano Mustard Yellow, Nyekundu, Kijani lakini hakikisha hizo rangi zinaendana na wewe usivae kitu ambacho hauko comfortable nacho. Ukivaa bold colors ni rahisi kuwa noticed kama ni muoga wa macho ya watu then usivae rangi zinazo shout sana.

  • Pattern

Ni sawa kuvaa pattern iwe stripes, pattern au checked, ikiwa wengi huwa tunavaa suit ambazo ni normal hazina mambo mengi unaweza kuwa watofauti kwa kuvalia suit yenye patterns tofauti tofauti itakufanya u-stand out.

  • Spice Things Up

Yes kuna njia nyingi za ku-spice suit yako kama unaweza kuvalia suspender,unawea ku-add belt kwenye blazer, kupaka makeup nzuri etc,hakikisha una kitu ambacho kinanyanyua muonekano wako na kukufanya uonekane wa tofauti.

  • Show Some Skin

Sio kwasababu upo kazini basi ndio ujifungie mwili mzima ufunge mpaka kifungo cha mwisho,miguu na mikono ifunikwe no,unaweza kuonyesha some skin kwa kufungua vifungo kadhaa vya shirt, kukunja mikono ya coat na hata kuonyesha skin kwa kuvaa suruali ya suit ambayo inaishia juu kidogo na kuonyesha mguu wako kiasi.

Well tunakutakia week njema.

Related posts