SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kutayarisha Stylish Outfit Za Week Nzima
Mitindo

Namna Ya Kutayarisha Stylish Outfit Za Week Nzima 

Kama wewe ni mmoja kati ya wale ambao tunaamka asubuhi na kuanza kufikiria tuvae nini, mwishoe tunaishia kuvaa chochote ili mradi tumevaa au kuishia kuchelewa tuendapo kwa sababu tu hatukuwa tumejitayarisha mapema.

Asikudanganye mtu a good & stylish outfit takes time to create, ni wachache sana wenye kipawa cha kufungua kabati na kuweza ku-create outfit inayoeleweka kwa muda mchache wengine tunahitaji muda na kuyafahamu mavazi yetu haswa, leo tunakuletea tips chache za kutayarisha stylish outfit za week nzima, sio tu zinakufanya u-save muda asubuhi lakini pia utaweza kuonekana stylish week nzima.

 • Tengeneza Nywele & Kucha Zako

Yes mtauliza afroswagga sasa nywele na kucha zitafanyaje niwe na stylish outfit, well bila nywele na kucha kuwa safi na kutengenezwa vizuri kwa hakika chochote utakachovaa hakitoonekana vizuri, kwahio hakikisha unatumia muda wako kwenda saloon kutengeneza nywele na kucha zako ziwe katika muonekano mzuri.

 • Safisha Viatu Na Pochi Zako

Kama ilivyo kwa kucha na nywele ni vizuri pia ukatumia muda wako kusafisha viatu na pochi zako, ni muhimu sana hivi vikiwa visafi ili kuubeba muonekano wako, hasa katika mapochi wengi huwa tunajisahau kuyasafisha. Pochi kama ni ya leather hakikisha umeifuta na inaonekana vyema kama ni ya vitambaa fua ili iwe safi.

 • List down occasions you will attend

Baada ya kufanya vyote hivyo, andika week hio unaratiba gani, utaenda wapi na wapi. Hii inasaidia kukufanya ujue vazi gani litafit wapi, oh yes ushawahi kujikuta siku unatakiwa kwenye event fulani lakini kwa sababu tu hukujiandaa mapema unavaa vazi ambalo hata haliendani na event? kuepuka hizi aibu ndogondogo hakikisha unajiandaa mapema kwa kuandika utaenda wapi ili wakati unachagua mavazi ujue lipi linafaa wapi.

 • Plan weekly / Day by day outfit

Wakati una plan day by day outfit zingatia vitu hivi vinne

 • Msimu – hii inakuja kwa hali ya hewa gani iliyopo / lakini pia inakuja katika fabrics, colors, & patterns zinazofaa kutumika kutokana na hali ya hewa iliyopo
 • Occasions – Kama tulivyoelezea juu jua utaenda wapi na kufanya nini hii itakusaidia ku-plan mavazi yanayoendana na uendapo
 • Formality – baada ya kujua msimu, occasion sasa uyaandae mavazi yako kutokana na hizo sehemu, kama formal event kama work meeting / meeting na mteja, kwenda kanisani etc, Semi – Formal events na informal event hizi zote unatakiwa kuzilist na kuandaa mavazi yake.
 • Activity – hii inaenda bega kwa bega na formality, ukishajua unaenda wapi basi pia utajua unaenda kufanya nini kama unaenda mahali ambapo unajua utakuwa unatembea kwa muda mrefu basi itabidi ubeba viatu vifupi etc.

Baa ya hapo kaa na kabati lako, anza kuchambua nguo moja baada ya nyingine na uplan ipi utavaa lipi na wapi. Cheza na kabati lako na jaribu ku-create mionekano mingine mipya, mix & match, lakini pia usiache kuzijaribu, isije siku ikafika ukazijaribu ukakuta labda kubwa au haikai kama ambavyo uli-imagine itakaaa.

well kama utajaribu hizi tips usisite kutumia hashtag yetu katika mitandao ya kijamii #afroclosetconfidence

Related posts

3 Comments

 1. youtube video download

  … [Trackback]

  […] Here you will find 12686 additional Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kutayarisha-stylish-outfit-za-week-nzima/ […]

 2. 카드수수료

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kutayarisha-stylish-outfit-za-week-nzima/ […]

 3. Test Automation tools

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kutayarisha-stylish-outfit-za-week-nzima/ […]

Comments are closed.