SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kutumia Mavazi Yako Ya Kila Siku Katika Mwezi Wa Ramadhani
Mitindo

Namna Ya Kutumia Mavazi Yako Ya Kila Siku Katika Mwezi Wa Ramadhani 

Ramadhani imefika na katika mwezi huu wengi huwa tunabadili aina ya mavazi, wengi tunajaribu kujifunika na kujistiri kuendana na mwezi huu. Basi kuna wengi ambao uhangaika katika swala zima la mavazi kununua mapya ili waweze ku-cope na mwezi lakini kumbe unaweza ukawa nayo ndani na unaweza kuyabadilisha kuendana na mwezi huu bila kutumia gharama nyingine.

leo tutakutajia baadhi ya mavazi ambayo unayo na unaweza kutumia mwezi huu.

 • Shirt Dress

Hatudhani kama kuna mwanadada ambae hana vazi hili katika kabati lake na kama huna basi si kosa unaweza kuwa na lingine tutakalo litaja hapo chini, unacho takiwa kufanya ni kuli-style kuendana na mwezi wakati miezi mingine ulikuwa unaweza kuvaa hivhivi bila kitu ndani mwezi huu unaweza kuvaa na suruali, skirt au ukalivaa kwa juu kama kimono ukafunga na mtandio wako ukawa umejistiri hujatumia gharama na bado modest.

 

 • Tuxedo Dress

Kama unayo na yenyewe ni msaada mkubwa kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani unaweza kuivaa kama long blazer lakini pia unaweza kuvaa kama shirt na suruali au skirt kwa ndani.

 • Turtle Neck Top

Zinapendwa sana hizi na zenyewe ni msaada mkubwa katika mwezi huu, unaweza kuvaa na skirt, suruali na hata gauni yenye mikono mifupi, kizuri kuhusu turtle neck top ukiivaa unaweza ukafunga kiremba kwa maana ina kustiri kifua na shingo kwa wakati mmoja.

 

culottes pants

Hizi ni zile suruali pana kwa chini ni kama fupi hivi, zipo so comfortable na wengi tunazo kwenye makabati, hizi nazo zinaweza kukusaidia mwezi huu unaweza kuzivaa na long sleeve top na mtandio vyema kabisa

 

Tutakuwa tuna wa update mara kwa mara ya jinsi unavyo weza kustyle vitu ambavyo unavyo tayari katika mwezi huu mtukufu.

 

Related posts

2 Comments

 1. all slot auto wallet

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kutumia-mavazi-yako-ya-kila-siku-katika-mwezi-wa-ramadhani/ […]

 2. weed delivery Toronto

  … [Trackback]

  […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kutumia-mavazi-yako-ya-kila-siku-katika-mwezi-wa-ramadhani/ […]

Comments are closed.