SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kuwa Dazzling Wedding Guest Bila Ya Kufilisika
Mitindo

Namna Ya Kuwa Dazzling Wedding Guest Bila Ya Kufilisika 

Kuwa mgeni mualikwa kwenye harusi kwasasa ni ghali, yaani ukisikia harusi unaweza kutamani Dunia ifunuke uingie, kuna michango kuna manunuzi ya sare, viatu, makeup, nywele, viremba, accessories na vingine vingi tuseme a wedding guest kwasasa inahitaji investment ya haja.

Well unaweza kuwa mgeni mualikwa ukapendeza lakini harusi ikiisha usifilike, leo tunakuletea Tips kadhaa za kuweza kuwa mgeni mualikwa uliyependeza bila ku-break the bank.

  • Anzakujiwekeza mara tu unapopata mualiko

Usisibiri mpaka mwishoni ndio uanze kuhangaika pa kupata hela ya michango na mavazi, hakikisha unajua unachokitaka mapema kitaku-cost shilingi ngapi na uanze kujiwekeza mapema.

  • Huitaji kununua sare kwa muhusika

Sasa hivi imetokea namna ambavyo wahusika wanauza sare, utakuta kijora cha sh 6000 kinauzwa 15,000 kwao au kitambaa cha 10,000 kinauzwa 30,000 na wanakukatia na meter kabisa 3 au mbili inawezekana wewe mwembamba hizo meter ni nyingi au una mwili zaidi hizo meter ni chache una poteza pesa nyingi. Jua sare take your time kuitafuta kwenye maduka ya vitambaa nunua inayo kutosha alimradi utokee kwenye sherehe umevaa sare yao.

  • Huitaji kwenda kushona kwa ma-designer

The pressure is real, siku hizi wenye sherehe wanakwambia kabisa tunafundi wetu au tuna designer wetu mkali anaweza kukushonea, au ukaona fulani alikuwa wedding guest kwa fulani akashona kwa designer basi na wewe uende. Unaweza kutafuta fundi mzuri mtaani ambae hana bei kubwa ukashona vazi lako na ukapendeza.

  • Shoes & Accessories

Kumbuka kununua viatu na accessories ambazo utazivaa tena na tena, sio ununue tu viatu ukavaa kwasiku hiohio na kuacha, nunua viatu na accessories ambavyo unaweza kurudia kwenye sherehe nyingine tena, hakikisha rangi za vitu hivi vinaweza kuingilia na sare nyingine nyingi mfano viatu vya silver au see through.

  • Makeup

Unaweza kupaka makeup yako simple as wewe ni wedding guest na sio mwenye sherehe, a simple yet nice makeup ambayo huitaji ku-break the bank maana makeup artist nao kwa bei Ma’shallah.

Related posts

2 Comments

  1. willy wonka chocolate

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kuwa-dazzling-wedding-guest-bila-ya-kufilisika/ […]

  2. read more

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kuwa-dazzling-wedding-guest-bila-ya-kufilisika/ […]

Comments are closed.