SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kuwa Stylish Huku Ukiendana Na Bajeti Yako
Dondoo

Namna Ya Kuwa Stylish Huku Ukiendana Na Bajeti Yako 

Wakati tunapitia mitandao mbalimbali tukakutana na story ya mwanadada aliyeingia katika madeni kisa tu ni kutaka kuwa Fashionista katika Instagram, Lissette Calveiro anasema watu walikuwa wakimuona anaishi maisha mazuri na kusafiri sehemu mbalimbali lakini nyuma ya pazia alikuwa ana mikopo na madeni ya $10,000/- sawa na Tsh 22,591,000.00/-   Lissette Calveiro “I was shopping…for clothes to take ‘the perfect ’gram”, she told the New York Post.“I was living above my means. I was living a lie and debt was looming over my head.”

Well hii imeturudisha kwa wenzetu na sisi ambao tunapenda kuonekana tumependeza na tunaishi maisha mazuri katika mitandao ya kijamii, inabidi uangalie uwezo wako na wapi unaweza kufikia na wapi huwezi. Unaweza kupendeza on a budget huitaji kuvuka kiwango chako cha pesa au kujirundikia madeni ili uonekane umependeza.

hizi ni tips tulizo kuandalia za namna unavyo weza kupendeza kulingana na bajeti yako

 • Ni Aina Gani Ya Mitindo Unapenda?

Kuna aina nyingi za mitindo kunawale wanaopenda kuwa chic, Vintage, Casual, Sexy, Corporate na nyingine nyingi, Hii itasaidia unapoenda kufanya shopping uweze kuchagua mavazi unayo yapenda na kukufanya uyavae kila mara. Kuna watu wengi ambao hawajui styles zao chochote wanacho kikuta wananunua na mwishoe huishia kuwekwa katika kabati bila kutumiwa hii inafanya utumie fedha nyingi katika mavazi ambayo huyatumii.

 • Kagua kile ulicho nacho

Tumia muda wako kukagua kile ulichonacho katika kabati nini huna na nini unacho, nini kinafaa kutolewa na kipi kinahitaji kuongezwa hii itasaidia kukufanya uwe na kabati friendly na kutokutumia fedha nyingi kuongeza vitu ambavyo kumbe unavyo tayari.

 

 • Epuka Trends

Epuka trends kwa maana zinakuja na kuondoka, kuliko kutumia pesa yako katika trends ambazo zinakaa mwezi au miezi kisha kupotea ni bora ukanunua basic pieces ambazo zinadumu muda mrefu, vitu kama Jeans, White Shirt’s, T-shirts, Pumps, Blazer etc ambavyo unaweza kuvitumia zaidi ya mara moja kwa namna tofauti na muda mrefu.

 • Be Timeless

Kama ambavyo tumesema hapo juu nunua vitu ambavyo vinaishi, Black Pumps, Little Black Dress etc hivi vinaweza kutumika mara nyingi, vinaishi kwa muda mrefu na katika kununua haya mavazi huitaji kununu ya gharama sana kuna mitumba na kuna wale ambao hawarudii mavazi unaweza kuwa unaongea nao na wakakuuzia kwa bei ya chini kulingana na kipato chako.

 • Wekeza katika Ubora

wengi huwa tunasema hapana siwezi kununua shirt ya zaidi ya elfu 20,000/- wakati naweza kupata kama hizo kwa elfu mbilimbili, ni kweli zinapatikana lakini je zina ubora? lipi bora kuwa nazo nyingi ambazo zina haribika kwa muda mchache na zimechakaa au bora kuwa na mbili ambazo zinadumu kwa muda mrefu? Unaweza kununua mtumba lakini uwe quality. Always chagua Quality Over Quantity.

 • Shop Sales, Clearance, and Off Season

Always kuwa karibu na maduka, wauzaji wengi wa mavazi huwa wana fanya sales, clearance na off season kuuza bidhaa zao kwa bei ya chini. Hii inakupa nafasi ya kununua kitu bora lakini kwa bei ya chini zaidi. hakikisha iko kitu ni timeless unaweza kukivaa tena na tena kwa sababu kama ni trendy hata kama umekipata kwa bei nafuu hakito kaa kwa muda mrefu.

 

 

Related posts

6 Comments

 1. my explanation

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kuwa-stylish-huku-ukiendana-na-bajeti-yako/ […]

 2. แทงบอลออนไลน์

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kuwa-stylish-huku-ukiendana-na-bajeti-yako/ […]

 3. boat movers near me

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kuwa-stylish-huku-ukiendana-na-bajeti-yako/ […]

 4. Psychedelic mushrooms Oregon

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kuwa-stylish-huku-ukiendana-na-bajeti-yako/ […]

 5. briansclub

  … [Trackback]

  […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kuwa-stylish-huku-ukiendana-na-bajeti-yako/ […]

 6. blog here

  … [Trackback]

  […] There you can find 12646 additional Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-ya-kuwa-stylish-huku-ukiendana-na-bajeti-yako/ […]

Comments are closed.