SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Za Kujenga Kabati (Wardrobe) La Ndoto Zako
Mitindo

Namna Za Kujenga Kabati (Wardrobe) La Ndoto Zako 

Wengi tunafikiri kujenga kabati ( wardrobe) la ndoto zetu ni ngumu, wengi huwa tunawaza kweli kuna watu ambao wanachukua muda wao kujua nini wanataka kuvaa maisha yao yote? kweli kuna mtu ambae kila siku akiamka anajua avae nini au anapata cha kuvaa katika kabati lake bila kuwaza sana? ina sound impossible lakini ukweli ni kwamba kuna watu ambao wapo serious sana linapo kuja swala la mavazi na hao ndio tunawaita fashionista’s au kusema mtu huyu yupo stylish. Hii ni kutokana na wao kujua wanataka nini kwenye kabati lao na nini hawataki na kuwa wana li-update mara kwa mara. Kama wewe ungependa kuwa mmoja wao soma njia hizi chache za kukuwezesha kupata kabati la ndoto zako

Sote tuna style’s mbalimbali wengine wapo more casual wale wa jeans na t-shirt kwa sana, wengine chic, punk, vintage etc. Kujua style yako kutakuwezesha kujua nini unatakiwa kuwa nacho katika kabati lako. Wengi ina tugharimu hapa unaweza kuona vazi zuri iwe mtu amevaa limempendeza au umeliona dukani ukalitamani na kununua kumbe vazi hili sio style yako linaishia kuvaliwa mara mbili au moja na kuendelea kukaa kabati tu, ukijua style yako ina punguza usumbufu huu na kuweza kukufanya ujenge kabati lako ambalo litaendana na wewe.

Basic outfit’s ni muhumu sana katika kujenga kabati la ndoto yako na ni kwa sababu unaweza kuzivaa na chochote unaweza ku-style basic  outfit vyovyote unacho hitaji ni kujua what are your basic outfits,kama ni casual utahitaji more of white t-shirt na jeans kama ni chic una hitaji white shirt na pencil skirt’s japo pia unaweza kuwa na jeans kwenye chic na pia jeans kwenye chic kama ambavyo tumesema basic outfits zinaingiliana karibu kwenye styles zote.

 • Focus katika kabati lako kuwa Remixable 

Kuwa na statement pieces ni sawa lakini usifanye kabati lako likajaa statement pieces kiasi ambacho hujui nini uvae na nini maana vyote vina make a statement kama ambavyo fashionistas wengi husema katika siku yako hakikisha unavaa one piece ambayo ni statement nyingine ziwe basic, nunua mavazi ambayo yanaweza kuingiliana na kufanya yale ambayo ni statement yakapoa au kuyapooza lakini pia kuyapa yenyewe nafasi ya kuwa kiungo kikuu na kukufanya uweze kuyavaa mara kwa mara na mara nyingi uwezavyo.

 • Jua Malengo Yako

Wengi wetu huwa hatujiwekei malengo wakati wa kununua vitu hasa mavazi,kila tunacho kiona kinatupendeza machoni tunanunua unaweza kujikuta una mavazi mengi ya aina moja hii ni kutokana na kutokuwa na malengo, Unatakiwa kujua una suruali ngapi ndani, t-shirts, gauni n.k na kujua nini ambacho kina miss katika kabati lako hii itakusaidia kuwa na mavazi tofauti tofauti unapo enda kununua mavazi unajua kabisa leo nanunua skirts kwa maana ndizo zinamiss kabatini hii inakufanya uwe na kabati ambalo lipo vizuri kila sekta

 • Wekeza Katika Accessories 

Accessories zinauwezo mkubwa wa kubeba vazi lako kuanzia blazer kufanya outfit yako iliyopo casual kuwa smart, statement necklace kufanya lile gauni lako lililo kuwa plain ku-pop nakadhalika unacho hitaji ni kuwa na accesories ambazo zinaweza kunyanyua mtoko wako.

baadhi ya accessories muhimu ni: Miwani, Belt, Statement Necklace, Pete< Mikoba etc


Kuna tips nyingi nyingi lakini hizi ni chache ambazo ni muhimu, unaweza kuongezea nyingine hapo katika box la comment.

 

Related posts

3 Comments

 1. description

  … [Trackback]

  […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-za-kujenga-kabati-wardrobe-la-ndoto-zako/ […]

 2. quality dope

  … [Trackback]

  […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-za-kujenga-kabati-wardrobe-la-ndoto-zako/ […]

 3. Order DMT online Perth

  … [Trackback]

  […] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-za-kujenga-kabati-wardrobe-la-ndoto-zako/ […]

Comments are closed.