Jinsi ambavyo miaka inavyo enda ndivyo jinsi ambavyo mambo yana badilika, style zinabadilika lakini do we have to change kutokana na muda? au tujaribu kukifanya kile tulicho nacho kiendane na wakati? tunadhani kubadilisha ulicho nacho kuendana na wakati ni jibu sahihi kabisa. Basi tuliona mwaka 2017 ulivyo kikuza kitenge jinsi ambavyo wabunifu na fashionista mbalimbali walivyo jaribu kukitumia. Its 2018 na tunaona inabidi tu move kwenye kuvaa full kitenge na kujaribu kukisyle kisasa well fashionista styleconnaisseur anatuonyesha namna gani unaweza kuchanganya kitenge na mavazi mengine.
Fur is so 2018, tumeona imevaliwa mara nyingi sehemu mbalimbali na watu maarufu mbalimbali hapa Fashionista Angel Obasi a.k.a styleconnaisseur akiwa amevalia fur black top na kitenge pants, akiwa amemalizia mtoko wake na satement chain, handbag na flat sandals, mtoko huu ni mzuri kama unaenda kukutana na marafiki na casual appointments.
Stripes , zipo katika trend kwa sasa na we would never thought unaweza kuvaa bold stripes na ruffle kitenge top ukapendeza hivi, this look is so bold na ina shout look at me, amevaa mavazi yake haya akimalizia na tassel earrings (trending) na favorite handbag yake. well unaweza kuvaa hivi kwenye mikutano ambayo unakutana na creative people.
A kitenge crop top? yes please, ame pair crop top yake ya kitenge na skin jeans ya blue, amemaliza muonekano wake na gray pumps, small waist bag, glasses na colorful tassel earrings. unaweza kuvaa huu mtoko kwenye mitoko ya usiku na marafiki (drinking & dancing)
Off shoulder kitenge top , Off shoulder ilikua on trend mwaka jana its not bad kama tukavuka nayo 2018, amevaa a colorful off shoulder kitenge top na traouser yenye mipasuo meupe amemalizia muonekano wake na gold open heels, kipochi cha pink na tassel earrings.
Sheer kitenge top well tutaandikia hii sheer na kitenge seems like itakiki sana mwaka huu maana imeonekana sana katika runways za Africa, amevaa top yake ya purple (color of the year) na suruali nyeupe.
Muonekano upi umekuvutia zaidi? usisite kuacha comment yako hapo chini.
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-za-kustyle-kitenge-kisasa/ […]
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-za-kustyle-kitenge-kisasa/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/namna-za-kustyle-kitenge-kisasa/ […]