Sote tunajua huu ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ndugu zetu waislam wanafunga. Jana Wasafi Tv wakishirikiana na mwanadada Zamaradi Mketema wame fturisha baadhi ya watu maarufu na ambao si maarufu lakini lengo kubwa kabisa la hafla hii ni kuzindua kipindi kiitwacho Nyumba Ya Imani katika channel yao. Well kulikuwa na red carpet ambapo watu maarufu wengi walipita. Wengi walipendeza na mavazi yao na 2 dubai collections walitisha sana katika kuwavalisha.
Wengi walivaa mabaibui na ma dish-dash kama kawaida, hakuna ambae tulimuona alijaribu kidogo kuvaa stara bila kuvaa mavazi hayo mawili lakini wapo ambao walipendeza zaidi ya wenzao haya tuone basi nani alipendeza na nani kwetu tuliona hapana.
Tukianza na currently mother mjengo, Hamisa Mobetto yeye hakutaka kabisa kufunikwa au kuwa sawa na wengine aliamua kuvaa hii gauni ya kijani na gold kutoka kwa mbunifu ab_design, Hamisa alivaa gauni hilo na remba la gold. akimalizia na makeup yake ambayo alipaka na bold lipstick. Tumependa muonekano yes sana lakini it was a Iftar event kwetu kama hii gauni ni too much sana ila amependeza.
Tukija kwa Diamond Platnumz mwenyewe alipendeza akiwa amevalia kanzu nyeupe yenye urembo wa vifungo kwa mbele, blazer ya rangi ya khakhi, huku akimalizia muonekano wake na eghal, amemaliza muonekekano wake na men sandals na miwani, katika wanaume Diamond au Naseeb Abdul ametop list yetu kwa waliopendeza.
Kwa wanaume anafuatiwa na Young Dee ambae yeye alivaa two pieces black outfit,amemalizia muonekano wake na eghal na saa na miwani. tumependa muonekano huu kwake unaendana na umri wake, mavazi yame m-fit vizuri & a perfect outfit for iftar hajazidi wala kupungua.
Kwa wanawake wa pili alikuwa Video Vixen Irene ambae yeye alivaa gold & black dress iliyo m-fit vizuri, amemaliza muonekano wake na simple makeup na trending big circle hoop earrings za gold, Irene alistand out na kuwa tofauti na wengine na gauni yake japo na yeye alilitoa 2 Dubai Collections lakini taste yake ilikuwa tofauti. Tumependa.
Mwingine ambae tulipenda vazi lake ni Wema Sepetu yeye alivaa maasai print kimono ambacho ali-match na kiremba chake, ndani alivaa gauni jeusi akamalizia na hoop kubwa za gold na make up by laviemakeup, Wema alivalishwa na Elisha red Label.
Aika Navykenzo nae alipendeza na hii Abaya yake nyeusi yenye urembo wa gold amemaliza muonekano wake na gold strap heels, Gold ilitawala sana katika Iftar hii
Ambao kwetu walituangusha ni Harmonize ambae yeye alivaa Kanzu ya rangi nyeusi, hii rangi imempoteza kwa maana yeye mwenyewe rangi ya mwili wake ni nyeusi, lakini pia Harmonize alivaa viatu vidogo red carpet jamani? hata kama hafla imefanyika sehemu ambayo umeizoa linapokuja swala la red carpet make no mistake.
Mwingine kwa upande wa wanawake ni Queen Darleen, Queen ana art ya kufanya nguo nzuri ionekane kawaida, anaweza akaia-accessorize ovyo au akaishusha uzuri wake. hapa alivaa hii gauni ya pink ambapo yeye peke yake ndio tulimuona nayo kama angaivaa vizuri kwa ku- accessorize vizuri na kufunga vizuri hijab angependeza sana but as usual she chose to go on the bleh list
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Here you will find 37522 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/nani-amependeza-na-nani-ametuangusha-katika-red-carpet-ya-nyumba-ya-imani/ […]