Weekend iliyopita kulikuwa na siku ya Mama Duniani ambapo Aunty Ezekiel aliamua kufanya Premiere ya movie yake iitwayo Mama siku hiohio wasanii mbalimbali walihudhuria akiwepo Diamond Platnumz, lakini pia tuliwaona Bongo movies wengi wakifika kum-support mwenzano, wengi walipendeza kutokana na tukio. Kulikuwa na red carpet of course watu walitakiwa kupendeza.
Mwenye hafla yake ambae ni Aunty Ezekiel na familia yake waliamua kuvaa Nigerian Theme ambapo kama na mwanadada Wema Sepetu angehudhuria na yeye alivaa Nigerian Wear. Kwa bahati mbaya hakufanikiwa kwenda.
Well imetokea maneno inasemaka Wema Sepetu na Faiza Ally wanajibishana nani alikuwa sahihi katika kuvaa mavazi siku hio?
Faiza Ally Alianza kwa Kuandika katika Instagram yake kwamba baadhi ya watu walivaa mavazi ya harusi Cinema
Wema Sepetu alijibu kwa kusema kuna watu walivaa mavazi ya Disco katika premiere ya movie ya mama katika siku ya mama duniani
kama fashion ambassodor tumeona ni vyema kama tukifananua zaidi kuhusu ili swala, wote wapo sahihi katika mavazi inategemea na jinsi ambayo wao wamechukulia ukubwa wa hili swala.
Tukianza na Faiza Ally – Faiza yeye aliichukulia simple kama movie date akaamua kuvaa double denim outfit na crop top nyeupe na Silhouettes za nude, ambapo alipendeza kwa kweli na ni perfect kwa movie date, kizuri ni kwamba alivaa heels akapaka makeup hakuonekana too casual kwa red carpet so hakuwa katika wale waliopendeza sana na wala waliochukiza she was so-so, lakini pia kwa maneno ya Wema Sepetu kwamba kavaa nguo za club Faiza ana body nzuri ambayo kuvaa vile ruksa. Flaunt it if you have it kuwa mama haimaanishi usijipende.
Kwa Wema Sepetu yeye aliamua kulibeba kuikubwa zaidi na kuvaa ki-mama kuendana na siku hio alipendeza na outfit yake ya ki-Nigeria, makeup yake on point na kwa sababu mwenye movie ni rafiki yake wa karibu akaamua kuwa sawa nae as mara nyingi huwa wanafanya hivyo, kwa upande wa maneno ya Faiza kwamba alivaa nguo za harusi ni kwamba hata wakina Lupita Ngong’o wakienda kwenye movie premiere wana pendeza na kuvaa miburuzo, kwahio Wema, Aunty Ezekiel, Hamisa wote walikuwa sawa kutegemea na wao walivyo beba uzito wa siku na movie yenyewe.
Well tupe maoni yako wewe unaonaje?
Related posts
HOT TOPICS
We need to have some sort of bima ila for enjoyment. Yaani wanakata ka % ka mshahara kako unakua na card ukienda se… https://t.co/W9oDoaN2YY
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…