SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Nguo Nyingi Lakini Unakosa Cha Kuvaa
Mitindo

Nguo Nyingi Lakini Unakosa Cha Kuvaa 

Nguo zimejaa kabatini, kwenye hanger na begi limejaa ila ukiambiwa upangilie nguo kumi kwa ajili ya mitoko inakuwa shida. Unabadili na kubadili, hii nguo haiendani na ile na hii haina blauzi ya kuvalia. Yani ni full kutaabika mpaka kuvaa inakuwa mtihani. Ushajiuliza ni kwanini una nguo nyingi lakini kupata a full look inakuwa shida? Basi hapa utajua kwanini unakumbana na hili tatizo na namna ya kulitatua.

 

 • Una Nguo Nyingi Zisizo Na Ubora 

Wanasema quality over quantity. Ni bora kuwa na nguo chache zenye ubora kuliko kujaza begi lako na mitumba third class iliyopauka, yenye matobo na alama. Nguo bora yenye rangi inayong’aa na kitambaa kizuri itakufanya uonekane uko smart na pia itafanya uonekane ni mtu anayejijali. Next time ukienda kununua nguo jaribu kununua vitu kutokana na ubora na sio udogo wa bei au wingi wa nguo. Ukinunua nguo kisa ni bei ndogo lakini haina ubora basi utajikuta unaiweka tu ndani. Utakua unashangaa kuona ulivyo na nguo nyingi lakini kila nguo unaona haifai.

 

 • Huzingatii Rangi Za Nguo Na Nakshi ( Accessories ) 

Wengi wetu tukienda kununua nguo hatutilii maanani suala zima la rangi. Tunanunua nguo ili mradi tu inavutia machoni. Kesho na kesho kutwa unajikuta una sketi nzuri sana lakini kila blauzi haikai. Au umevaa nguo ila rangi ya viatu haitoi ushirikiano hivyo unaamua uvue uvae nyingine tu. Jitahidi kujua rangi za nguo zako na rangi unazopendelea zaidi. Ukiwa unanunua nguo jaribu kufikiria utaivaa na nini au uinunulie nini ili ipendeze.

 

 • Haununi Nguo Za Mtukio Mbalimbali 

Nadhani ushawahi kuona watu ambao kwenye matukio wao ni wazee wa kuharibu dress code, inawezekana na wewe ni mmoja wao. Yani kwenye dinner date mtu kavaa nguo ya ofisini, harusini kavaa nguo ya club yani mipangilio ya mavazi ni kama vita kuu ya dunia; kila kitu kipo kisipotakiwa. Hapa tatizo kubwa linakuwa ni mtu hanunui mavazi kwa ajili ya matukio mbalimbali au hajui avae nini kwa wakati gani hivyo unakuta mtu analazimisha kuvaa chochote atakachoweza ili mradi amefika kwenye tukio. Kuna watu wanavaa gauni ndefu kama Cinderella na ametolewa kwa ajili ya chakula simple cha jioni na mtu. Tafadhari usijitie aibu mara kadhaa jitahidi kununua nguo mbili tatu za matukio kadhaa kama nguo ya sherehe ya harusi, party na marafiki, club, mikutano ya kimaendeleo, red carpet na matukio mengineyo usije ukajikuta unavaa satin club.

 

 • Huna Basic Pieces 

Basic pieces ni zile nguo muhimu sana kuwa nazo. Yani hizi nguo ni rahisi kuzichanganya na nguo nyingine ili kuleta muonekano mzuri. Baadhi ya basic pieces ni T-shirt nyeupe na nyeusi, gauni jeusi liwe linafika magotini, koti la langi inayoendana na rangi nyingi, wallet, miwani ya jua, scarf au mtandio, Jeans inayokutosha vizuri ya blue, suruali nyeusi ya kitambaa, raba nyeupe,nyeusi au kijivu, flats za wazi na zinazofunika, sketi nyeusi na vest(tank top). Hivyo sio vyote kuna vingine vingi ambavyo ni muhimu sana na ukiwa navyo basi hata kama umevaa suruali umekosa top utakimbilia “basic piece”juuau umevaa top huna nguo ya chini basi utachukua basic piece ya chini uvalie.

 

 • Hauwekezi Kwenye Nakshi  (accessories)

Kuna baadhi ya nguo zinachohitaji tu ni accessories sahihi na basi unaweza kukamilisha look. Kabla hujakatia vazi lako tamaa jaribu kuwaza ukiongeza mkoba gani, kofia gani, miwani gani, hereni, cheni au viatu gani itapendeza. Inawezekana unakosa tu vitu vya kunogesha muonekano wako ndio maana kila nguo unaona haivutii. Basi Jitahidi kununua vitu kadhaa ili kuzipandisha nguo zako hadhi.

 • Hujajua Mwili Wako Unataka Nini 

Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nikinunua nguo zilizovutia kwenye macho yangu lakini wakati wa kuvaa nilikuwa napitia mateso ya kisaikolojia. Unajua ile mtu unajiuliza ni nini hiki kimo ndani ya hii nguo. Lakini makosa hayo yalikuja kunifunza kuwa tumeumbwa tofauti na kila mmoja ni mzuri na anavutia kwa namna yake lakini usijaribu kufanya kitu kwa kuwa tu kimekubali kwa mtu mwingine. Nilipokuja kujitambua basi imekuwa rahisi na imepunguza makosa wakati wa kuchagua mavazi. Jitathmini, jua una umbo aina gani, ingia google na mitandao mingine kama pinterest kujua mwili wako unapendeza mavazi gani. Nguo zako za zamani zikiwa ndogo kwako au zikizeeka basi gawa inawezekana mwili wako umebadilika na hauwezi kupendeza tena kwenye nguo hizo. Usilazimishe kuiga trend, yani ile mitindo inayoenea kwa kasi na watu wengi wanaiiga. Kama trend inaendana na mwili wako basi iga ila kama haikupi sapoti basi potezeaa au fanya kuiboresha iendane na wewe.

I hope umejifunza. Sio lazima kubadili kila kitu kwa wakati mmoja. Unaweza kuanza kujirekebisha taratibu kwa kubadili tabia moja baada ya nyingine kila unapoweza na ipo siku utajikuta una kabati yenye nguo ambazo hazikupi shida kutengeneza muonekano fulani. Kumbuka kupendeza huanza kwa kujipenda, kukubali usichoweza badili na kujiamini, as they say, “Confidence is the best outfit.”

Imeandikwa na @Raymimie

Related posts

4 Comments

 1. linked here

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/nguo-nyingi-ila-huna-cha-kuvaa/ […]

 2. สร้างเว็บไซต์

  … [Trackback]

  […] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/nguo-nyingi-ila-huna-cha-kuvaa/ […]

 3. edible gold chocolate bar

  … [Trackback]

  […] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/nguo-nyingi-ila-huna-cha-kuvaa/ […]

 4. Strawberry Mochi 3.5g Flower

  … [Trackback]

  […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/nguo-nyingi-ila-huna-cha-kuvaa/ […]

Comments are closed.