SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ni Sawa Mwenza Wako Kukuweka Mipaka Katika Mavazi?
Mitindo

Ni Sawa Mwenza Wako Kukuweka Mipaka Katika Mavazi? 

Hili swala huwa linatokea Mara nyingi majumbani kwetu, wengi wanakatazwa au kupewa mipaka ya nini wavae na nini wasivae na wenza wao, hii hutokea pale tu mwenza anapo penda mwenza wake avae Mavazi ya aina Fulani na si ya aina Fulani na ni kutokana na Sababu tofauti, Inawezekana Kuwa ni wivu au kutokupenda aina hio ya Vazi.

Katika kudumisha mahusiano yoyote ni jambo la kawaida kwa wenza kutafuta namna ya kushahabiana, hii ni kwasababu wawili hawa wamaweza kuwa wanatokea kwenye mazingira yenye tabia na imani tofauti tofauti lakini licha ya hivyo hata linapokuja swala la mapenzi na ushabiki katika baadhi ya vitu kamwe hamuwezi kufanana na hii ndio maana halisi ya binadamu hatufanani

huyu anaweza kuwa anapenda hiki hiliihali mwenza wake asikipende ni jambo la kawaida na wala sio dhambi wala kosa mara nyingi busara hutumika katika kutafuta uhiano huo, aidha mmoja akiache kitu anacho kipenda au mwingine ajifunze kukikubali anacho kipenda mwenzie yote hii ni katika kutafuta uwiano na usawa ili mpate kuishi kwa amani na upendo.

Inawezekana ni mambo madogo madogo lakini leo tunalenga katika mavazi na style Swali linakuja je ni sawa kwa mwenzi wako kukuchagulia nini uvae? Je hii haiingilii Uhuru wako binafsi? Come to think si ni kwamba alikukuta ukiwa unavalia Mavazi ya aina hio Kwanini sasa hivi mko Kwenye mahusiano ayakatae na kutaka uvae Mavazi ya aina fulani yanayo mpendeza yeye?

Kwetu tunaona hupaswi kumchagulia mwenza wako mavazi au style, hupashwi kumuwekea mipaka katika kile ambacho yeye anakipenda na umemkuta akikifanya mwisho wa siku mahusiano yanapaswa kuwa katika kupeana uhuru na kuaminiana, unapo mkataza mwenza wako asivae vazi la aina fulani sababu tu wewe unaona wivu au halikupendezi ni kumnyima uhuru wake katika ulimwengu wa fashion na style lakini pia kumsononesha kwa kushindwa kuvaa kile ambacho moyo wake unapenda.

Tupe maoni yako je ni sawa au si sawa mpenzi wako kukuchagulia mavazi?

Related posts

2 Comments

  1. cz firearms for sale

    … [Trackback]

    […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/ni-sawa-mwenza-wako-kukuweka-mipaka-katika-mavazi/ […]

  2. hidden cam fuck bbw

    … [Trackback]

    […] Here you can find 49076 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/ni-sawa-mwenza-wako-kukuweka-mipaka-katika-mavazi/ […]

Comments are closed.