Wakati bado hatuja olewa sote huwa tuna ndoto za namna ambavyo ungependa gauni lako la harusi liwe lakini pale unapopata nafasi ya kuchagua gauni mara nyingi huwa tunapata panic attack, nitavaa nini? rangi gani? nitapendeza? vipi kuhusu kufunikwa na wageni waalikwa? Hizi ndizo tips chache tulizo kuandalia za kufanya wakati unachagua vazi lako la harusi
- Anza Kutafuta Gauni Lako Mapema
Kuanza kulitafuta mapema kutakupa nafasi ya kupata options nyingi ambazo unaweza kuchagua taratibu kipi kina kufaa, ukichelewa kulitafuta utapata shida na kuchagua lolote ambalo litakuwa mbele yako ili mradi siku ipite bila hata ya kulipenda.
- Jua location
Unapojua sehemu ambayo harusi yako inafanyika ni rahisi kujua unavaa nini, kama inafanyika kwenye hall basi utachagua vazi linaloendana na sehemu husika kama ni ufukweni al kadhalika unajua uvae nini, hii itakusaidia kukupa urahisi wa wewe kuchagua vazi lako.
- Jua style yako
Linapo kuja swala la style ni wewe upo comfortable na gauni la aina gani, usinunue gauni sababu lipo kwenye trend au kwa sababu marafiki zako wamekwambia zuri, hapana tafuta ambalo wewe unaendana nalo na hata siku ya kuja kuonyesha picha zako kwa watu utakuwa huna regrets, mwisho wa siku ni siku yako na sio yao.
- Fitting’s fitting’s
Fanya fittings mara kwa mara na hii ni muhimu kwa sababu kuna ma bibi harusi ambao wanatabia ya kunenepa na wengine kukonda kabla ya harusi kwahiyo ni vyema ukawa unaenda kujaribu vazi lako kila baada ya week kadhaa ilikujua kama linakutosha au lah, sio siku inafika nguo haiingii au ina pwaya.
Hizi ni zile ambazo hutakiwi kifanya.
- Husiwaache watu wakuchagulie vazi lako
Kama ambavyo tulisema juu, ni siku yako wewe ndio unatakiwa kuchagua vazi ulipendalo, unaweza kupata ushauri kwa watu mbalimbali lakini usiwafanye wao wachague vazi wanalo dhani ni sawa wakati kwako si sawa.
- Husiji – limit
Tafuta mavazi ya aina mbalimbali, ukianza mapema basi utapata muda wa ku-explore zaidi, kuanzia rangi si lazima wote tuvae nyeupe, design’s etc, chukua muda wako ku – explore madukani, mitandaoni ili uweze kupata kilicho bora.
- Usinunue kwa sababu ni trend
hata kwenye mavazi ya harusi kuna ambayo yana trend kwa wakati huo, please don’t buy sababu ni kitu ambacho kina trend muda huo usifuatishe mkumbo nunua kile ambacho unaona kinafaa na kitakuwa timeless kwako kwamba ukikiangalia hujutii nilivaa tu kwasababu ya trend bali utasema this is exactly what i wanted.
Well ni matumaini yetu tips zitakusaidia please tuambie na nyingine ambazo unadhani zinaweza ku-fit hapa
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/nini-ufanye-na-nini-usifanye-wakati-wa-kuchagua-gauni-la-harusi/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/nini-ufanye-na-nini-usifanye-wakati-wa-kuchagua-gauni-la-harusi/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/nini-ufanye-na-nini-usifanye-wakati-wa-kuchagua-gauni-la-harusi/ […]