SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia Za Kuupenda Mwili Wako
Mitindo

Njia Za Kuupenda Mwili Wako 

Ni rahisi kuwaangalia wengine na kuwaadmire miili yao, kuona kuwa wako vizuri, wanapendeza wakivaa chochote, tofauti na mimi. Unaweza ukangalia staili za nguo na kuona itawapendeza wengine ila sio wewe. Kuna kipindi miezi inapita bila kujiangalia kwenye kioo, na ukijiangalia unaona ile sehemu moja tu, sehemu ambayo utajaribu chochote iliuibadilishe.

Kuna kipindi nilikuwa nauchukia mwili wangu, nauonea aibu, na waonea wivu wale ambao hata wale nini hawabadiliki. Naangalia miguu ya fulani, na mikono ya mwingine, na nawish ingekuwa yangu. Nikivaa sijisikii comfortable, najisikia aibu, navaa ili nisiwe uchi, naona kila mtu anaona tumbo langu, kila mtu anaona jinsi mwili wangu ambavyo haukosawa. Sikujiona mrembo, nilikuwa natamani niufiche mwili wangu, kwani ulikuwa unanifanya najisikia vibaya, ukilinganisha na maslay queen walivyo.

Niliteseka sana kwenye kipindi hicho sometimes nilikuwa nakataa hadi mitoko kwasababu nawaza nitakayeenda naye atanionaje, nawaza navaa nini ambacho kitaficha ‘madhaifu’ yangu, ni bora nibaki tu niufiche huu mzigo nilio nao, ambao ni mwili wangu. Nilikuwa navaa nguo za mikono mirefu ili kuficha mikono, sinyanyui makwapa maana sitaki ile sehemu ya mwili ionekane, navaa nguo ndefu maana naonea aibu viunga vya mwili wangu, lakini pia naweza mapozi ya kunionyesha uso fulani, na filter kibao zinazoniedit uzuri ambao sio wangu ili tu nionekane watofauti.

Watu wengi tunaopishana nao wanachukia miili yao, wengine wanachukia rangi waliyonayo, wengine wanachukia kwasababu hawana vitu vinavyoonekana kuwa ndio uzuri, wengine wanachukia kwasababu wanatamani viungo vyao vingebadilika au visingekuwepo hivyo vilivyo kwenye miili yao.

Iwe kwasababu yoyote ile, naelewa hisia unayopitia, na natamani nikushirikishe vitu vilivyonisaidia mimi kuwa comfortable na mwili na vile nilivyo leo, mpaka nimefikia kutokujali hata watu wanasemaje, kwasababu najipenda mwenyewe nilivyo. Mambo hayo ni:

  • Kuona na kuthamini kazi ambayo mwili wako unaifanya

Jamani miili yetu inapitia mengi sana kwaajili yetu, sana. Na kumbuka kuwa bila mwili wako, usingekuwako. Sio tu mwili wako ni wewe, bali mwili wako unafanya vitu vingi ambavyo usingekuwa hivyo ulivyo au usingekuwepo visingefanyika. Nilipogundua mambo ambayo mwili wangu unayafanya, nikaanza kuuthamini, na kuuonesha upendo na kuwa kind to my body. Kuna wengine wanachukia size waliopokiasi kwamba wanatamani wapungue leo leo, ila kumbuka kuwa mwili wako unajua unachokifanya, kuna muda unafanya unayoyafanya ili kukuweka wewe uwe hai.

  • Jua kuwa huo ndio ulionao

Sometimes tunajisikia vibaya kwasababu ya kujilinganisha, matangazo na mitandao ya kijamii huchangia. Kumbuka kuwa wenye matangazo hufanyaa hivyo kukutia presha ununue bidhaa yao, na kumbuka kuwa social media watu huwa wanapost yale wanayoyaona mazuri kuhusu wao. Kwenye maisha haya huo ndio mwili ulionao mpaka kifo, je isingekuwa bora ukaspend muda huu kuujua na kuupenda hivyo hivyo ulivyopewa? 

  • Kuzipenda sana sehemu unazoziona wewe nzuri

Ukianza kuappreciate sehemu ambazo kwako unaziona nzuri, utaziona sehemu nyingine pia kwa jicho la tofauti. Kwamba sio mbaya kama unavyofikiria. Kwamba utofauti wako ulionao ndio unaokufanya uonekane mzuri, kwamba kuna wewe hivyo ulivyo mmoja tu duniani

  • Nyamazisha sauti za wengine 

Watu husema vitu bila kujua vinakuumaje au upo kwenye hali gani. Watu husema vitu kutokana na wao walivyo na sio wewe ulivyo. Ukiambiwa comment kuhusu mwili wako usiichukue personally, sometimes watu hupenda kuumiza wenzao. Nyamazisha au jitenge kabisa na pages Instagram au watu wanaokuambia mwili wako haufai.

  • Own your body

Ukishajua huu ndio mwili wako, nakutafuta kuupenda vile ulivyonao na kuuona kama zawadi inayokusaidia kufanya mambo mengi, na kuuona kama wewe, ukafikia hatua ya kujipenda kabisa, own your body. Tembea kwa kujiamini, there is only one you. Vaa kwa kujiamini, cheka kwasababu meno yako hivyo hivyo yalivyo ni yako na tofauti na ndio yanayokupa utofauti, dance kwa vile mwili wako ni wa muhimu kwako. Own your body. Jiangalie kwenye kioo, jiambie wewe ni mzuri, ukipewa comment nzuri iandike, iweke sehemu, jikumbushe kuwa wewe ni mzuri, na unafanya hayo unayoyafanya kwasababu ya huo mwili.

  • Pia usikilize mwili wako

Mwili wako ni wewe, ndio sababu uko hai mpaka leo. Usikilize mwili wako unapokuonesha signs zozote zile zichukulie serious na ufuatilie.

Eunice💜

Napenda Ice cream na kuandika. Naandika katika blogu inayoitwa abiblegirl.com.

Related posts

6 Comments

  1. How you can learn to love your body // 5 Tips - Eunice Tossy

    […] post was first posted on AfroSwagga, in […]

  2. How you can learn to love your body // 5 Tips – Eunice Tossy

    […] post was first posted on AfroSwagga, in […]

  3. แทงมวย

    … [Trackback]

    […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/njia-za-kuupenda-mwili-wako/ […]

  4. บ้านมือสอง

    … [Trackback]

    […] Here you will find 89397 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/njia-za-kuupenda-mwili-wako/ […]

  5. Gun SHOP USA

    … [Trackback]

    […] There you can find 97568 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/njia-za-kuupenda-mwili-wako/ […]

  6. buy mushrooms online

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/njia-za-kuupenda-mwili-wako/ […]

Comments are closed.