SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Office To Date Night Outfit Ideas
Mitindo

Office To Date Night Outfit Ideas 

It’s friday na wengi huwa tunaalikwa mitoko ya usiku siku hii, japo ijumaa ni siku nzuri ya kutoka kuna kuwaga na tatizo la mavazi hasa kwa wale ambao tunaona uvivu kutoka kazini kwenda nyumbani kubadilisha halafu twende kwenye hio date na ukifikiria foleni njiani basi unaamua kughairi au kukata tamaa, well say yes to the date leo tunakupa tips za jinsi ya kuvaa ofisini na ukitoka hapo unabadilisha vitu vichache ambavyo unaweza kubeba kwenye pochi yako na kuvaa kwenye date.

  • The Little Black Dress 

 

Moja kati ya essentials tano unazotakiwa kuwa nazo a little black dress nayo ni moja wapo, ni very helpful pale unapotaka kutoka na hujui nini cha kuvaa lakini pia its flattering, kama una date unaweza kuvaa a little black dress na mkoba wako, blazer na heels. Kisha ukabeba a nice clutch na accessories za usiku ukitoka unavua blazer na kubeba clutch, ongezea accessories na makeup na nywele uziweke ki-date date then you good to go.

  • High Waist Trouser 

Hizi nazo zina work magic katika pande zote mbili mtoko wa ofisi na usiku, unaweza kuvaa high waist trouser yako ofisini na shirt au blouse ya choice yako, usiku ukatoa shirt na kuvaa a crop top, achia nywele kupata a casual & sexy feeling, beba clutch na ongezea accessories

  • Pencil Skirt 

Zenyewe kama high waist trouser pia zina cheza vizuri pande zote mbili, tunacho pendea pencil skirt ni ile sexiness inayokupa na kuchora umbo yako vizuri hapa inapendeza zaidi kama inakuwa ile bandage pencil skirt kuliko zile za vitambaa

Unaweza kuvaa jumpsuit, culottes na mavazi mengine ni namna tu ya wewe kucheza nayo ki-ofisi na baadae kuja kuwa date night outfit, kumbuka kubeba makeup na perfumes maana ukitoka kazini kama huto rudi nyumbani zitakuwa zimesha isha kazini inabidi uziongezee, matumaini yetu tumekusaidia leo.

 

Related posts