kwa jina la cheti cha kuzaliwa anaitwa Mickson Amos, lakini wengi tunamfahamu kama Mr Outfit Mickson ndivyo anavyo jiita huko Instagram (@mr_outfit_mickyson), Mickyson ni celebrity stylist ambae amesha fanya kazi na watu wengi maarufu akiwepo young dar es salaam, lakini pia alikua stylist wa mashindano ya bongo star search leo tupo nae kujua mawili matatu kuhusu yeye na maoni yake katika style na fashion za hapa kwetu Tanzania
Afroswagga : Tuambie kwanini ulichagua styling? whats so special about it ulikiona ndani yake?
Mr Outfit : Style ni ubunifu ambapo unapata nafasi ya kuchagua muonekano wako kulingana na mazingira uliyopo na Style haipotei wala haichuji ni lifestyle. pia style si kwa mavaz na muonekano tuu bali katika kila nyanja ya maisha yetu.
Afroswagga: Mteja wako wa kwanza super star alikuwa nani na ilikuaje?
Mr Outfit : Kwanza Kabisa Asilimia Kubwa ya wateja wangu ni Ma SuperStar. Nakumbuka Kama sikosei Mwaka 2009 kama sio 2010 mwanzoni. Youngest Artist wakati huo Na mwenyewe uwezo Mkubwa kisanaa. Anaitwa Young Dee na kazi yake Ya kwanza ya Teacher nilifanya nae na Mimi ikiwa kazi yangu Ya kwanza Kabisa iliyo nitambulisha.
Young Daresalama Nilifahamiana nae BRITISH CANCER ilikuwepo posta karibu na Chuo cha IFM kipindi hicho. Nakumbuka Kila jumapili kulikiwa na shows pamoja darasa juu ya vitu mbali mbali Kuhusu Muziki sana sana wa Hip hop. Kwasababu nilikiwa Mdogo kimri kulingana na watu walikuwa wenye Sanaa wakati ule nilitafuta Mtu ambae ingekuwa rahisi kwangu kunielewa na KUKUBALI kufanya nae Kazi.
Afroswagga : Tofauti ya Stylist Mickson na Stylist wengine ni nini?
Mr Outfit : naweza kufanya kazi na mtu yoyote Yule.
Pia kuwa mkweli na muwazi kwa mteja wangu kama nguo haifai au hatopendeza kulingana na mwili wake ama umbo au mahali anapoenda. Huwa na weza solve tatizo linapotokea kwa wakati muhafaka. Mwisho kabisa nilijiendeleza kusomea ninachokipenda. Nina Elimu na kazi yangu Advanced Diploma in Fashion Designing, Apparel Merchandising
Afroswagga : Kama stylist wa kiume tutajie 3 pieces muhimu mwanaume kuwa nazo katika kabati lake
Mr Outfit : Mkanda saa & wallet
Afroswagga : Kuna wanawake wengi sana wanafanya styling unawezaje kukeep nao kwenye industry?
Mr Outfit : style ni ubunifu na natumia kipaji changu kupambana na ushindan wa soko lote kwa ujumla
afroswagga : Kuna hili swala la wasanii wa kiume kuweka virasta au kuvaa bandana ina trend kwa muda sasa nini maoni yako? hakuna style nyingine bora kuliko hizi?
Mr Outfit : Me nadhani wengi wao hawana uelewa au elimu juu ya kuwa na muonekano unao kutambulisha kama celebrity. Kuwa wa kipekee wanapaswa wapate watu wenye skills kwenye fashion. Kama mimi hivi
Afroswagga : Tips ambazo una tumia kila siku kuonekana stylish?
Mr Outfit: Kwanza Kabisa kwenda na wakati nikimaanisha kujua vitu gani vipo kwenye trend Na kuvivaa pia coz ni rahisi kunitambulisha kama stylist… Kufanya mazoezi. Kusoma na kuwa na ufahamu na elimu zaidi kwenye kazi yangu.
afroswagga : Ukiambiwa uchague kabati la mtu maarufu ungechagua kabati la nani?
Mr Outfit :Hahahahaha kuna mtu anaitwa Gucci mane ni hiphop artist Wa America anatumia hela nyingi zaidi kutengeneza Muonekano wake na kununua every latest Style . Ila kabati la Davido pia kama linanihusu.
Afroswagga : Mtu gani maarufu unatamani kufanya nae kazi siku moja?
Mr Outfit :Mkurugenzi wa vipindi Cloudstv,Fm Ruge Mutahaba. Ndio mtu maarufu ninae Tamani kufanya nae kazi.
Afroswagga : Tumeona kazi yako katika wimbo mpya wa Young Dee Kiutani Utani take us through that road, nini kili kuinspire, outfit zilitoka kwa mbunifu gani? na kwanini black & white?
https://www.instagram.com/p/BY5V0mWHO62/?taken-by=youngdaresalama
First of all Aah. Lazima kuwe na communications nzuri kati ya director, stylist and artist.
Mara nyingi wazo au script huwa inatoka kwa director au msanii. Ila hii ilikiwa tofauti kidogo. Nilikuwa na a idea kichwani Muda mrefu but sikiwahi kupata Nyimbo inayoitaji concept ya Cars Racer Racing. Haikuwa kazi ngumu kutokana na aina ya mavazi yanayo valiwa kwenye Mashindano ya magari kwa wenzetu ni kitu kile kile ilibidi tukibebe. Ni sawa na kuambiwa tengeneza vazi la doctor au nurse ki kawaida linajulikana likoje.
Why Black and White: Usipoweka draft za black and white kwa Sex girl Racer speed itamchukua Muda mrefu Mtazamaji kuelewa concept ya video. Pia nawashukuru Twins fashion kwa kukamilisha mavazi ya video nzima na kufanya kazi kuwa nzuri zaidi.
Afroswagga : Kama stylist huwa unajisikiaje kumuona msanii maarufu kaenda red carpet au katupia picha mitandaoni akiwa hajapendeza na maoni yako?
Mr Outfit : Kama nilivyosema muonekano unamtambulisha mtu kabla ya kuongea neno lolote msanii anapoenda kwenye red carpet akiwa hajapendeza anaonekana haithamini kazi yake na hayuko makini unprofessional
Afroswagga : chochote ambacho ungependa kuwaambia watanzania wakike na wakiume kwa ujumla
Mr Outfit : me napenda kuchukua nafasi hii kwanza kuwashukuru Watanzania wote kwa ujumla kwa namna moja au nyengine. Siku hizi wamekuwa watu waku support vya nyumbani sana kama mtu ukijitangaza vizuri kwa kile ulicho nacho iwe bidhaa,fashion,music n.k. Pili Kwa vijana wenzangu Wajue kwamba hakuna Binadamu amezaliwa bila kuwa na kipaji chapekee. Kikubwa wasikate tamaa watumie muda mwingi kutafuta njia zitakazo wafikisha Mbali zaidi kupitia vipaji au taaruma zao
Special thanks kwa swalihi fashion week na awards zengine , Blogs Majarida vipindi mbali mbali vya Tv na Radio vyote vinavyotoa support Kuhusu Fashion kwa Ujumla
Related posts
2 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you can find 68017 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/one-on-one-na-celebrity-stylist-mickyson-amos/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 24832 more Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/one-on-one-na-celebrity-stylist-mickyson-amos/ […]