SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Angie Mtatiro Shares Tips On How To Walk In High Heels
one one one

Angie Mtatiro Shares Tips On How To Walk In High Heels 

Angel Alfred Mtatiro ni mshindi wa pili katika Miss Tanzania 2022/2023, ni moja kati ya ma’miss wenye mwendo wa kipekee hasa pale akivaa viatu virefu, mwendo huu tuliuona katika Jukwaa la Miss Tanzania umetuvutia na tukaona sio mbaya kama tukifanya nae mahojiano akatupa tips chache za kutembelea viatu hivyo.

Afs: Tungependa Kujua Historia Yako Kwa Ufupi?

Angel: Majina yangu kamili ni Angel Alfred MTATIRO .. Mimi ni mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2022. Nilizaliwa Juni 29, 1999 katika familia ya watoto 7 , mimi ni last born..I’m originally from Mara (Mkurya) ….Safari yangu ya maisha so far imejaa hatua muhimu na za kusisimua.Nilianza elimu yangu ya shule ya msingi Mwaka 2006 na kuhitimu kidato cha 7 mwaka 2012 ..Nilifahulu kwenda sekondari katika shule ya Oysterbay Secondary mwaka 2013 na kuhitimu mwaka 2016 kidato cha nne ..Pia nilifanikiwa kufahulu kwenda kidato cha tano na sita (Advance ) katika shule ya Mawenzi iliyopo Moshi, Kilimanjaro mwaka 2017 mpak 2019 .. Nikafahulu kwenda Chuo Kikuu cha Dar es salaam mwaka 2019 mpaka 2022 na kupata shahada yangu ya Biashara, nikibobea katika Utalii..

Nilianza safari yangu katika tasnia ya urembo mwaka 2021, niliposhiriki katika shindano la Miss Higher Learning, na kushika nafasi ya tatu. Mafanikio haya yalinifungulia milango, na kuniwezesha kushiriki katika shindano la Miss Tanzania 2022, ambapo niliheshimiwa kuwa mshindi wa pili. (Miss Tanzania 2022 first runner )…. Jukwaa la Miss Tanzania limekuwa muhimu katika ukuaji wangu binafsi. Limeongeza si tu ujasiri wangu, lakini pia limekuza ujuzi wangu wa mawasiliano, kunisaidia kufikia malengo yangu…….. Leo, nina bahati ya kufanya kazi na makampuni mbalimbali kama balozi na influencer . Nafasi hii imeniwezesha kuwa sehemu ya kampeni mbalimbali za brands na kuchangia katika mipango ya kuelimisha jamii.

Afs: Ni Moja Kati Ya Ma’miss Wenye Tembea Nzuri Sana, Ulianza Lini Kujifunza Kutembelea Heels?

Angel: Asante, Kutembea na heels nimeanza mda mrefu sana..Nakumbuka tangu nipo mdogo nilikua napenda heels Yan nguo ya skukuu haiwi kamili Kama sijanunuliwa viatu virefu ..😂😂 Kuweza kutembea na heels sio ngumu ila inabid tu iwe unavaa Mara Kwa Mara Ndio mtu anaweza kuwa comfortable na kuweza kutembea navyo vizur…

Afs: Wanasema Ni Vyema Kuanza Na Short Heels Kwenda Ndefu Je Kwako Ulianzia Inch Ngapi?

Angel: Kuanza na short heels ni ushauri mzuri sana Kwa wanaojifunza , mimi nlianza na wedges nlikua natembea nazo sana, Mara nyingi kanisani Kila jumapili npo na wedges zangu miguuni 😂 Baada ya kuvizoea Ndo nikaanza na inch 2 mpaka sasa nmeshazoea navaa kuanzia inch 4 kuendelea .

Afs: Ulishawahi Kuumia Au Kuanguka Wakati Unajifunza Kutembelea Heels?

Angel: Sijawahi kuanguka wakati najifunza kutembelea heels, Ila aina Hii ya viatu inahitaji uvumilivu sana ..Kipindi ambacho vilinitesa ni wakati tupo kambini kwenye mashindano yote nliyopitia Maana tunavaa heels asubuhi, mchana mpaka jioni , siku zote ambazo tupo kambin na pia mazoez na rehearsal zote tulikua tukifanya na heels inafika wakati miguu inachoka, nlipata muscle cramps Mara nyingi sana …Pia shida ya heels Kama sijavaa muda mrefu basi nikija kuvaa nikazurula nazo lazima miguu iume 😅😅

Afs: Tips 5 Unaweza Kumpa Mtu Anaeanza Kutembelea Heels

Angel: Anza na heels zenye inch ndogo ili uweze kuwa comfortable Kwa kua Ndo unaanza kujifunza

  • Jifunze kutembea kwa mstari mmoja..Unapotembea, weka mguu mmoja mbele ya mwingine kama unavyotembea kwenye mstari.
  • Zingatia posture yako , Hakikisha mwili wako unakua straight usiinamie mbele au nyuma.
  • Tembea taratibu usiharakishe. Take your time and be confident with each step you take..!
  • Fanya mazoez sana …Mazoezi ni muhimu. Anza kwa kuvaa heels nyumbani kabla ya hujatoka nje …

Afs: Tofauti Na Wengine Una Mwendo Relaxed Sana Ni Kama Unatembelea Flats, How Did You Get The Walk?

Angel: Mimi ni beauty Queen napaswa kutembea kwa utulivu na heshima kwa sababu inaonyesha kujiamini kwangu na kujistahi ….Kutembea nikiwa relaxed kunamaanisha kuwa mimi ni mtulivu na nipo comfortable in my own skin na Sina haraka. Kwahyo nimeweza kuwa na muondoko huo kwasababu nilizingatia hayo na mazoea ya kutembea na heels nakua tu relaxed …Wanasema Polepole Ndio mwendo

Afs: Je Ukiwa Unatembelea Heels Huwa Unafikiria Nini Mpaka Unakua Relaxed Vile?

Angel: I just live in the moment na kutembea tu Kwa kujiamini..😊

Afs: Tukiwa Tunaelekea Kwenye Miss Tanzania 2023 Una Ujumbe Gani Kwa Washiriki Wasasa Kuhusu Tembea Zao Jukwaani?

Angel: Ushauri wangu Kwa warembo wote wanaoshiriki Miss Tanzania 2023 ni

  • Jiamini, kujiamini kunaweza kufanya tofauti kubwa sana. Kumbuka, unapoingia jukwaani, wewe ni star!
  • Jiandae, Hakikisha umejiandaa vizuri Kwenye mavazi, make-up, na jinsi unavyotembea.
  • Onyesha personality yako and be your true self..Miss Tanzania sio tu kuhusu uzuri wa nje, bali pia uzuri wa ndani. Onyesha jinsi gani wewe ni wa kipekee!
  • Kuwa na furaha..Usisahau kufurahia Kila unachofanya . Kama unafurahia, basi hata watazamaji watafurahia pamoja nawe. Don’t forget to Smile 😊
  • Kumbuka kwa nini uko hapo..Kumbuka daima lengo lako na kile unachotaka kutimiza kama Miss Tanzania. Hii itakusaidia kuwa na motisha na kudumisha lengo lako. All the best Girls 🤍

Afs: Chochote Ambacho Ungependa Kuongezea Au Kuongea Na Watanzania

Angel: Urembo sio tu sura na umbo, bali ni kuhusu kujiamini, kuheshimu wengine, na kuwa na tabia njema. Kila mmoja wetu ana uzuri wake wa kipekee, na tunapaswa kuuthamini na kuutunza. Tujifunze kujipenda sisi wenyewe jinsi tulivyo, na tushiriki upendo na wengine… Pia tunapaswa kuthamini kila siku na kuitumia kikamilifu. Kumbuka, maisha ni mafupi sana, hivyo tufanye kila tunachoweza kuwa na maisha yenye maana na furaha. Hebu tujitahidi kufanya kazi kwa bidii, kuwa na roho ya kujitolea, na kuwa na mtazamo chanya. Kwa pamoja, tunaweza kufanya Tanzania yetu kuwa mahali pazuri zaidi…🤍

Related posts