SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Cyrill Kamikaze Talks About Fashion & Hygiene
one one one

Cyrill Kamikaze Talks About Fashion & Hygiene 

Cyrill ni moja kati ya wanamuziki wanaofanya vyema katika kazi zao lakini pia ni moja kati ya wale wachache wenye kujipenda na kuvaa vyema, tumepata nafasi ya kuzungumza nae machache kuhusu mitindo na usafi kwa wanaume,

AFS: Wengi tunakujua kama Cyril, tuambie kuhusu wewe background yako kidogo.

Cyrill: Naitwa Cyrill Fransisco known as Cyrill kamikaze. Ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto wa tano. Nimehitimu shahada ya kwanza katika chuo cha Institute of Social work. Ni mwanamuziki pia ni mfanyabiashara. Wengi wananifahamu kama msanii wa bongo fleva, ambapo nimeanza kujihusisha na muziki tangu nikiwa sekondary, lakini nikiwa form 3, nilibahatika kufanya wimbo wangu wa kwanza “Nipo juu” ambao ndio uliniweka kwenye ramani na kuanzisha safari yangu ya muziki rasmi.

AFS: Ni moja kati ya fashionable male celebrity Tanzania, lini ulianza kupenda mitindo na kupendeza?

Cyrill: Naweza sema Fashion ni kitu kipo ndani ya damu. Mimi sikuwahi kufundishwa au kuambiwa niipende fashion. Wakati naingia kwenye muziki, niliingia na style ya swagg yani hio ndio ilikua kama kiki yangu miaka hio, unapoongelea swagg na fashion basi unamuongelea Cyrill na Wakacha, ambapo wakacha iliundwa na mimi pamoja na Jux tangu tunasoma wote Green acres secondary. kila interview ilikua naongelea fashion na jinsi gani natamani wasanii wawe fashionable. Kwa sababu zamani wasanii hawakujali sana mionekano yao, mimi nikatamani hilo libadilike. Ilikua nikienda kwenye show wanasubiri tu leo atavaa nini? Na ndio maneno kama “Kutupia, Swagg ziko on, kuweka switch, Kupoa” ni maneno baadh kati ya niliyo yaanzisha mpaka leo yamekua maarufu kwa watu wengi. Nadhani nimekuwa balozi namba moja wa fashion Tanznaia kabla ya social media. Kipindi cha nyuma baadhi ya maduka yalikua yananitafuta nakuuliza kitu gani kipo kwenye trend walete since walikua na nafasi ya kwenda nje ya nchi kufuata mizigo.

AFS: Wa Africa tunaile mwanaume akipendeza tuna m-categorize kwenye group fulani, ulishawahi kupitia hili na ulideal nalo vipi?

Cyrill: Ndio, mwanaume kwa Africa akijipenda ni tatizo. Sio tu mavazi mara nyingine hata nyumbani ukiwa msafi ni shida, watu wanadhani uanaume ni kutojipenda wanaojipenda wanaaminika hawako busy na kazi, watu wakiingia kwako wakaona kupo vizuri, lazima watasema kitu, mimi imenikuta mara kadhaa na sababu moja, ni kwamba ilikua muda wote nataka kuwa nadhifu na kunukia poa, kwaiyo kuna namna nishaangaliwa kwa jicho lingine ila sikujali sana, lakini naimani kwa dunia ya leo wengi wamebadilika nakujua umuhimu wa utanashati.

AFS: Una skin care routine kama ndio tuambie kuhusu routine yako ( products unazotumia unaweza kuzitaja pia)

Cyrill: Hapana sina skin care routine, ngozi yangu haijawahi nipa stress sana. Although miaka ya karibuni kutokana na kubadili makazi ili leta shida kidogo. Ila sio jambo la kuleta msongo kama nilivyo sema.

AFS: Tuambie kuhusu matunzo ya nywele na ndevu, una rotine yoyote ya hivyo vitu kama ndio tuelezee (products unazotumia)

Cyrill: Kuhusu nywele, nazihudumia sana. Maana nimekuwa na nywele ndefu kwa muda mrefu. Natumia Olive products kuanzia shampoo mpaka mafuta yake. Zinafanya nywele zangu kuwa vizuri mara zote.

AFS: Una miliki perfume ngapi na kunukia vizuri ni muhimu kiasi gani kwako? (Unaweza kuzitaja if you dont mind)

Cyrill: Namiliki perfumes kadhaa.. sikumbuki idadi vizuri, kwa maana nina makazi tofauti kwaiyo waga naacha baadhi, na nikitaka kusafiri nabeba chache ambazo nazipenda zaidi, kwasababu napenda kunukia poa, mtu akinipa zawadi ya perfume nakuwa nafurahi zaidi kuliko hata mtu atakae nipa simu LOL, napenda ku explore dunia ya perfumes. Ninazo zikumbuka kwa haraka ni Tom ford Ombre leather , Arman Code, Invictus, One Million, Dolce & Gabanna, Sauvage Elixir, Sauvage dior, Terre Dhermes, Zara blue and silver, Bleu De Chanel, Mazarino blue, Creed Aventus, Polo Blue, Polo Red, Versace,Adidas, rare gold.

AFS: Lets play a game, what do you prefer?
Sneaker or boots?
Crocs or sandals?
Trendy or Classy?
Casual or formal?
Prints or monochrome

Cyrill: I prefer Sneakers

Sandals

Classy

Casual

Prints

AFS: Chochote ungependa kuwashauri wasanii chipukizi kuhusu mitindo na kujijali

Cyrill: Ushauri wangu mkubwa siku zote kwa wasanii chipukizi ni kwamba, Wewe kabla hata ya muziki wako ni BIDHAA, na jinsi utakavyo itengeneza na kuibrand vizuri bidhaa “WEWE” ndio jinsi bidhaa zako zingine kama muziki wako ambavyo utaenda vizuri. Kwaiyo wachukulie serious sana suala hilo.

Related posts