We are nestefied! Tulimuona media host kwenye fainali za BSS 2023 kapendeza sana hivyo Afro tuliweza fanya mahojiano na the man behind Meens’s wow looks
AFS: Tumeona previous collaborations toka kwako na Meen Ally and this is among the best. Waweza tuelezea the inspiration behind the dress and how long ilikuchukua kutengeneza the dress?
NESTE: HI, Afro. Well tulianza collaboration na Meena Ally toka mwaka 2022 kwenye fainali za Bogo Star Search. Alivutiwa na kazi zetu ana kutaka kuendelea nasi.
This time tumefanya naye kazi mbili. One outfit for the red carpet (the red) and nyingine for the show. (the yellow) The inspiration behind outfits hizi ni pamoja na mwezi February kuwa mwezi wa mapenzi na msimu wa Valentines. Hii ni for the red dress.
The yellow ball gown dress, well Meena anapenda sana ball gowns. Hata ukimshonea nguo mbili, moja ataomba iwe ball gown. So nikachagua the color choices to fit the theme and mood.

AFS: With a busy timetable na muda ukiwa sio rafiki, fittings zilifanyika ndani ya muda gani?
NESTE: Muda uliotumika kushona nguo ni siku mbili. Siku iliyofuata ilikuwa kumalizia the last-minute details lakini vingi vilifanyoka ndani ya siku mbili ukiondoa zile siku za Kwenda kutafuta the needed materials.
Kwa kweli muda huwa ni mdogo, at the moment hapa at Neste hakuna a big staff ya kusema kuna mtu atashona, mwingine atafanya pattern making, mwigine atafuata materilas or fittings so sometimes inakuwa very tricky, unatakiwa kuwa sehemu nyingi kwa wakati mmoja.
Baada ya siku mbili za kushona, tuliweza fanya fittings na fittings zilifanyika once, hakukuwa na marekebisho makubwa labda small touches za hapa na pale

AFS: Experience yako on dressing and designing Meena Ally ikoje? Wamuelezea kama client wa aina gani?
NESTE: Meena is a cool client. Anakupa uhuru wa kuweza kutengeneza kitu kizuri bila restrictions. Lakini pia ni mtu mwenye taste anayefahamu vitu, hasiti kukuelekeza pale anapoona kitu hakijakaa sawa.
AFS: Waweza share na sisi previous looks and designs ambazo umewahi fanya for Meena Ally?
NESTE:BSS finals 2022, nguo mbili ikiwemo ball gown nyeusi
Event ya Clouds, nguo ya lavender, mid length

AFS: Zamani ulikuwa unafanya pia menswear lakini miaka ya hivi karibuni umebase na female wear? Why? Na male designs ndio mwisho wake?
NESTE: Yes, zamani tulkuwa tunafanya nguo za kiume na za kike at the same level. Kwa sasa tunafanya lakini kwa kiwango kidogo. Kilichotokea ni kwamba Neste ilikuwa ni partnership ya watu wawili lakini mwenzangu alifariki, na ndiye aliyekuwa akideal sana na nguo za kiume 100%. So bado najaribu kuirudisha iwe at the same level kama mwanzo
AFS: 2023 ndio kwanza imeanza, what’s your vision kwa mwaka huu? Tutegemee nini?
NESTE: Yes, 2023 imeanza na nilitamanikuanza mwaka with a bang, and nashukuru nimeweza fanya hilo. So namshukuru Mungu my plans zimeenda accordingly. Hii ni post yangu ya kwanza toka maka uanze na nimepokelewa vizuri beyond na nilivyotarajia. Imenipa moto wa kufanya vizuri na kuendelea mbele Zaidi.
AFS: And celebrities gani in Tanzania ama abroad ungependa kumvalisha, awe nestefied?
NESTE: Ningependa kufanya kazi na Zuchu. Nimeona ananiulizia so natumaini atakuwa nestefied na nitakachomvalisha. Pia natamani kumvalisha Sishikii, she has the perfect body ya kuwa nestefied. Pia Irene Uwoya na Jacqueline Mengi ambapo hapa kwa nitakuwa nimeweka tivk kwenye my checklist.
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you will find 36661 additional Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/one-one-one/neste-talks-about-dressing-meena-ally-at-bss-2023/ […]