Elizabeth Michael “Lulu” alipata nafasi ya kutuwakilisha katika Africa Magic Viewers Choice Awards ( AMVCA ), Event ilifanyika huko Lagos, Nigeria. Toka Eliza apost ata-attend hii event kila mtu alikuwa excited kuona atavaa nini na sisi tukiwepo.

Eliza alivaa blue dress kutoka kwa mbunifu Kyamirwa. Tunaamini wote wawili wangefanya kazi nzuri zaidi ya hii, tumeshaona kazi kali kabisa kutoka kwa Kyamirwa & perfect choices kutoka kwa Elizabeth. This was just off.

Material ni ya kawaida sana, the design it self haikuwa kwa ajili ya mtu mfupi imefanya details zote kuonekana zimekaa sehemu moja, tofauti na ambapo angevaa mtu mrefu ingekuwa tofauti. Too much un-necessary details, tunadhani walitaka gauni iongee lakini badala ya kuwa statement gauni imekuwa unattractive, Kuanzia kwenye cleavage, puff sleeves,high slit, pleated hapo kwenye hips too much going on.

The worst part ya hii gauni kwetu ni mbele kwenye hips, we truly wonder ni kitugani kilikuwa kinatakiwa kutokea hapa, the details are not-clear na hii ndio sehemu ya mbele ya dress ambayo ilitakiwa ikaevizuri ivutie.

Tulitamani kuwekwa kwenye top 10 za best dressed na wabunifu wetu wajitangaze pia lakini imekuwa tofauti kabisa na matarajio yetu.

Tukiwa tumemaliza kuongelea kuhusu hii gauni let’s us give some few solutions ambazo tunaweza kufanya siku nyingine tukialikwa na kuhudhuria event kama hizi

  • Andaa vazi mapema & work hand in hand na designer. Kuanzia fittings, nguo inatakiwa kuwaje na kama inafaa kwa umbile lako.
  • Designer think outside the box, kuanzia kwenye materials, tuachane na ubahili satin zipo kuanzia za elfu tatu mpaka thelasini angalia na hii nguo inaenda kuvaliwa wapi na material gani inahadhi ya sehemu hio.
  • Stylist Stylist Stylist, ukiangalia wenzetu asilimia 95 walishirikiana na stylist katika mavazi yao ya siku hiyo na red carpet iliwaka moto kwa maana kila mmoja alifika amependeza.