Miss Tanzania imefanyika Ijumaa ambapo warembo 20 walichuana vikali na hatimaye tukampata mmoja ambae ataenda kutuwakilisha Miss World itakayo fanyika Tarehe 14 December 2019 Jijini London, Uingereza.
Miss Tanzania 2019 Ni Sylvia Sebastian Bebwa ambae anatoka mkoani Mwanza, ana umri wa miaka 19 na ni mwanafunzi ambae anasomea computer maintenance and repair

Wengi wameonekana kutokukubaliana na ushindi wake na tunaweza kusema tunaelewa frustration ya wengi, Sylvia alipatwa na kitete katika kujibu swali kwenye shindano, hapa inabidi apewe somo kubwa sana kabla hajaenda Miss World anatakiwa apewe somo la public speaking, na namna ya kujibu swali.
Sylvia alichagua kujibu swali kwa lugha ya kiingereza baada ya hapo alishindwa kulielewa swali vizuri kama kunauwezekano wa kumpa mkalimani ni vyema zaidi akaenda nae au Miss World wawe notified mapema kwamba Sylvia anaweza lugha ya kiswahili zaidi kama kunanamna ya ku-solve hili swala ianze kufanyiwa process.

Aanze kuandaliwa mapema kuanzia national costume, makeup & hair team, viatu na mavazi atakayovaa Miss World yaandaliwe mapema kama kuna uwezekano wa kutafuta watu wampe sponsorship ya hivi vitu basi process ifanyike mapema.
Tusisubiri mpaka tarehe za mwishoni ndio aanze kuwa coached inabidi tuanze kuspot na kurekebisha matatizo madogo madogo aliyokuwa nayo mapema na kum-shape zaidi ambapo anapaweza azidi kuwa mkali zaidi.
Otherwise congratulations to Sylvia lakini pia Miss Tanzania Committee mwaka huu onesho lilikuwa zuri maandalizi yalikuwa vyema.
Rai yetu kwa umma wa watanzania na watu wote wanaofatilia tasnia ya mitindo, ubunifu na urembo ni kwamba, mashindano ya miss Tanzania kwa mwaka huu yamekwisha hivyo wote kwa pamoja tuunganishe nguvu na kumsupport Sylivia ili apate kutuwakilisha vema kwenye jukwaa la Miss World. Nadhani badala ya kumshambulia na kuiharibu taswira yake kwenye mitandao ya kijamii tunaweza kabisa kuijenga na kuiimarisha kupitia majukwaa hayo hayo. Ushindi wa Sylvia Miss World ni watazania wote, hivyo tufanye kwa ajili ya Tanzania.
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Here you will find 31470 more Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/our-two-cents-to-miss-tanzania-committee/ […]
… [Trackback]
[…] Here you will find 30823 more Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/our-two-cents-to-miss-tanzania-committee/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 27317 additional Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/our-two-cents-to-miss-tanzania-committee/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/our-two-cents-to-miss-tanzania-committee/ […]