Afroswagga imefanya mazungumzo na mbunifu Hameed Abdul mbunifu anae chipukia kwa kasi anae fanyia shughuli zake za ubunifu mkoani morogoro, Tumefanya mahojiano nae kuhusu kazi yake ya sasa aliyoitoa kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Eid.
afroswagga- tuelezee kidogo kuhusu wewe na lini umeanza ubunifu?
Hameed- mimi naitwa Hameed Abdul, nilianza kudesign tangu nina umri wa shule ya msingi lakini kujitumbukiza katika fashion industry ilikua ni mwaka 2011, kuanzia apo nikashiriki katika mjukwaa mengi Tanzania na Nje.
Afroswagga- JE? una fanya kazi za kiume au na za kike pia?
Hameed- Actually napenda sana kudesign nguo za kike, na naona naweza (kitu hiki watu wengi hawafahamu) ila ni kazi kutafuta, na design nguo za KIUME na mara chache za kike, usije ukashangaa next collection zikiwa za kike tupu, jibu nafanya nguo za KIUME na za kike kwa mbali.
Afroswagga- nimeona katika collection yako ya Eid na Ramadhani umetumia rangi za pink na nyekundu nini kime ku-insipire kutumia rangi hizo? maana ni mara chache kwa wavulana kutumia rangi hizo
Hameed- Rangi hizi zote zinatumika kwa mwanaume, kilicho ni inspire kutumia rangi ya pink na nyekundu ni kuweka ladha ya mwonekano wa collection yangu.
Afroswagga- JE? ni kwanini uliamua kubuni mavazi ya Eid na Ramadhani wakati ni ya muda mfupi yaani mwezi mmoja?
Hameed- nimebuni mavazi ya Ramadhani na Eid ili clients wangu wapate mavazi mazuri na tofauti katika kipindi hiki, lakini pia mavazi haya unaweza kuvaa muda na kipindi chochote inategemea na sehemu.
Afroswagga- Ni ugumu gani unapata ukizingatia unafanya kazi mkoani?
Hameed- kiukweli ugumu ninao upata ni kuwa mbali na clients wangu,kwa sababu wateja wangu wakubwa wapo dar na nje ya Tanzania na mikoa mingine
Afroswagga- Je kuna chochote unataka kuwaambia wateja wako na Watanzania kwa ujumla?
Hameed-napenda kuwaambia watanzania kuwa tupende vya kwetu nikiwa na maana fashion industry Tanzania imekuwa na designers wanafanya vizuri katika tasnia ya ubunifu ndani na nje ya nchi.
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-hameed-abdul-mbunifu-kutoka-morogoro/ […]
… [Trackback]
[…] Here you will find 8041 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-hameed-abdul-mbunifu-kutoka-morogoro/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-hameed-abdul-mbunifu-kutoka-morogoro/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-hameed-abdul-mbunifu-kutoka-morogoro/ […]