SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Pata Kumjua Josh Ipyana Mshindi Wa Master Tanzania 2019
Mitindo

Pata Kumjua Josh Ipyana Mshindi Wa Master Tanzania 2019 

Shindano la Master Tanzania liliweza fanyika mwezi huu kwa mara ya kwanza nchini, na Josh Ipyana
kuibuka mshindi, Master Tanzania 2019. Ili kuweza kumtambua na kulielewa shindano tuliweza zungumza naye:


AFROSWAGGA: Waweza tuelezea Master Tanzania 2019 lililenga kutafuta kijana wa aina gani?
JOSH: Master Tanzania ni shindano linalotafuta kijana,umri wa miaka 18-29 mwenye ujasiri, akili pamoja na kipaji chenye upekee. Kipaji ndo kitu muhimu sana.


AFROSWAGGA: Mshindi wa Master Tanzania 2019 huzawadiwa nini?
JOSH: Wanatafutwa washindi watatu kama 1 st runner up, 2 nd runner up pamoja na Master Tanzania mwenyewe. Washindi watatu wataungana mwisho wa mwezi October kuelekea Hollywood Marekani kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao.


AFROSWAGGA: Kipaji chako kilichokuwezesha kuonekana ni kipi hadi kushinda?
JOSH: Kipaji changu ni muigizaji wa sauti ama voice over artist. And yes, ni mwanamitindo yaani model.


AFROSWAGGA: Pia umekuwa ukifanya unamitindo (modelling). Je ulianza lini? Ulishawishikaje? Na experience yako ya kwanza on the runway ilikuwaje?
JOSH: Nilianza kufanya mitindo mwaka 2017 so now ni miaka miwili hivi. Nilishawishika kwasababu napenda sana mitindo na kilichonitia nguvu ni kwamba nina vigezo vyote so hata wakati naingia haikua ngumu kupata nafasi kwenye shows kubwa. Ndani ya mwaka mmoja nikapata nafasi katika jukwaa kubwa la Swahili Fashion Week.


AFROSWAGGA: Any favourite designers ambao ungependa fanya nao kazi/umeshafanya nao kazi?
JOSH: My favorite designer is Martin Kadinda. Ni mtu ambaye Mungu amempa moyo wa upendo,huruma, heshima na busara na ni msaada mkubwa sana kwa hata wanamitindo wengi nchini.


AFROSWAGGA: Changamoto zozote ulizokutana nazo kazini? Na miaka 5/10 unaionaje tasnia ya uanamitindo? Tutaweza fikia nchi kama Sudan/Nigeria zenye wanamitindo wakubwa duniani?
JOSH: Changamoto zipo nyingi sana lakini ndo tuanaelekea tunashukuru tunaanza kuona support kutoka serikalini… Basata wameanza kua karibu na watu tasnia ya mitindo. Naamini ndani ya miaka miwili ijayo Tanzania itakua miongoni mwa nchi tatu zinazotoa wanamitindo wazuri na ghali zaidi africa. Kwa sasa tuna zaidi ya wanamitindo 5 wanaofanya vizuri nje ya nchi kama vile Flaviana matata, Abel Kipaso, Thomas nguka, Josephine Mumwi pamoja na Zara Bedel

Interview by @willibard_jr

Related posts

5 Comments

  1. БИРЖА КРИПТОВАЛЮТ

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-josh-ipyana-mshindi-wa-master-tanzania-2019/ […]

  2. best puppies for sale in southdakota

    … [Trackback]

    […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-josh-ipyana-mshindi-wa-master-tanzania-2019/ […]

  3. 티비위키

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-josh-ipyana-mshindi-wa-master-tanzania-2019/ […]

  4. why did my morning glory seeds die

    … [Trackback]

    […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-josh-ipyana-mshindi-wa-master-tanzania-2019/ […]

Comments are closed.