SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Pata Kumjua Na Kupata Skin Tips Kutoka Kwa Hellen Dausen “Nuya’s Essence”
Mitindo

Pata Kumjua Na Kupata Skin Tips Kutoka Kwa Hellen Dausen “Nuya’s Essence” 

Kwa wale msiomjua Nuya jina lake kamili ni Hellen Dausen  aliwahi kuwa Miss Miss Universe Tanzania 2010, Hellen Dausen ambaye  ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Nuya’s Essence Nuya’s Essence ni kampuni ya vipodozi asilia vya mwili kama sabuni,mafuta etc, Mwaka jana Hellen alitajwa na jarida la Forbes kama Afrika kama wajasiriamali wenye umri wa chini ya miaka 30, wanaopewa kipaumbele kuwa mabilionea siku za usoni.

Afroswagga- tuambie kidogo kuhusu nuya essence?

Nuya- Nuya’s Essence ni kampuni inayo jihushisha na kutengeneza vipodozi asili kwa kutumia mikono. Vipodozi hivi hutumia malighafi za asili kama mimea mbali mbali, miti shamba pamoja spices za aina tofauti. Asilimia kubwa ya malighafi hizi hutoka hapa hapa nyumbani Tanzania na chache hutoka nje ya Tanzania. Nuya’s Essence ina ofisi maalum huko visiwa vya Zanzibar, Unguja pamoja na duka letu la kwanza pale Stone Town. Bidhaa zetu ni nzuri sana kwa ngozi za aina zote, watoto, na hata wakina mama wajawazito. Kwa sasa tuna mwaka wan ne kwenye biashara na namshukuru Mungu sana tunaendelea vizuri kuelelimisha wanawake kutumia vipodozi asili kujitunza kwa maisha ya kila siku.

Afroswagga – Katika biashara zote kwanini natural products kwa ajili ya ngozi?

Nuya -Mimi ni mpenzi sana wa natural products na hii imesababishwa na Mama yangu mzazi, alikuwa anatupakaa sana mafuta ya nazi au olive oil kila siku na kutwa akisema ni mazuri sana kwa ngozi, kwa hiyo nimekuwa nikijua hivo na mpaka sasa hakuna mafuta ninayotumia kwa wingi sana kama Mafuta ya Nazi. Na yanasaidia ngozi yangu kuwa ng’aavu, yenye afya na nzuri muda wote. Na vile vile wakati nilipata hili wazo la kutengeneza vipodozi asili mwaka 2013, kulikuwa hakuna watu wanafanya hii biashara vizuri, kwa umakini ambao ningependa uwepo, kwa hiyo nikaona nijikite, nioneshe utofauti na kutengeneza bidhaa bora inayokubalika.

Afroswagga – Una ngozi nyororo japo ni ya asili je ni matokeo ya product zako? kama yes unaweza kutupa skin care routine yako?

Nuya- Ndio, mimi nimeanzan kutunza ngozi yangu kwa kutumia vitu vya asili kabla hata sijaanza kuviuza. Na mpaka sasa kabla sijatoa product yoyote sokoni lazima niitumie mwenyewe kwanza kwa mda mrefu, nikishirikiana na marafiki zangu wa karibu pia na familia yangu ili kunipa mrejesho kama bidhaa ni nzuri au mbaya na nifanye marekebisho gani.

Ndio: nina skincare routine ambayo nimeiandika kabisa na kubandika ukutani ili nisiwe nasahau au kuruka routine sana maana mambo ni mengi. Huwa lazima nishe uso mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kabla ya kulala. Kwa asubuhi: nasosha kwa sabuni ya Charcoal kutoka Nuya’s Essence, napakaa Rose Toner (hii husaidia kusawazisha skin PH), napakaa eye cream, alafu Serum, alafu napakaa oil (Nuya’s Essence 100% Pure Coconut Oil), alafu napakaa sunscreen, lipbalm, alafu lipstick nyekundu, Napenda sana lipstick nyekundu. Huwa sipakai sana make-up labda niwe na shughuli muhimu. Kwa usiku: Baada ya kuosha, napakaa uso Rose Toner, alafu serum, alafu mafuta ya nazi, napakaa na mask ya usiku. Kila wiki mara tatu huwa nasugua mwili na uso na Body scrub ya Nuya’s Essence ya Lemongrass Seaweed. Na pia huwa napakaa mask usoni mara mbili au tatu kwa wiki. Siku za wikiendi ambazo nakuwa na mda mwingi, ndio natengeneza mask asili nyumbani kutumia matunda au mboga au chochote, mchanganyiko ninanoupenda sana ni: Asali, manjano, mtindi, limao na mafuta ya Tea Tree. Pia huwa natumia sana barafu, kuitembeza usoni baada ya kuosha uso ili ngozi ya uso ikaze vizuri na kuzuia makunyanzi mapema.

Afroswagga – katika ulimwengu huu wa kujichubua nini kilikuvuta mpaka kuanzisha biashara ya natural.

Nuya -Nimeona wanawake wengi wakihudhurika sana na hii mikorogo, na hivo ikanilazimu kuwa natoa mafunzo na kuwaelekeza jinsi ya kutunza ngozi zao na zikapata ung’aavu mzuri ambao ni zaidi ya kuwa hata mweupe. Na pia kuwaelimisha madhara ya madawa haya makali. Na hivo ikawa kama mvuto wa ziada kwa kazi yangu. 

Afroswagga –  tunaona upo natural kuanzia nywele hadi ngozi je una products za natural hair pia?

Nuya -Kwa kweli product zetu tumezielekeza sana kwenye utunzaji wa ngozi lakini kama unavoona katika kila product imeandikwa pia inaweza kutumika kwenye nywele pia. Mfano, mafuta yetu ya Raw Shea butter ambayo ni mazuri sana kwa nywele, mimi binafsi huyatumi sana kufanya nywele zangu japo ni ndogo lakini ziwe na afya na zisikatike ovyo. Pia mafuta ya nazi, ni mazuri sana kwa nywele, hivyo product zetu ni nzuri sana kutumika kwenye nywele pia.

Afroswagga – katika kutengeneza product zako huwa una fikiria watu wenye matatizo ya ngozi labda akitumia mafuta ya nazi ana haribika ngozi na una kabiliana nayo vipi ili kuweza kuwasaidia?

Nuya – Kwa kweli kila mtu ana ngozi tofauti na kweli kuna wateja wachache ambao mafuta ya nazi ngozi zao hazikubali kabisa japo ni natural, kwa hiyo tuna mafuta mengi mengine ambayo mteja anaweza kujaribu na ikawa sawa kwa ngozi yake. Tunaelewa kuwa kuna watu watakuwa na allergy na mafuta kadhaa na hivo tunajaribu kuleta mafuta ya aina mbali mbali ili aina moja ikiwa haifanyi kazi vizuri basi anaweza kujaribu mafuta mengine mpaka akapata yale yanayompenda. Ukiangalia sabuni zeti zimeandikwa zinasaidia matatizo ya ngozi Fulani, kama Charcoal soap, husaidia ngozi ya mafuta, Goat Milk soap, husaidia ngozi kavu….ndio, huwa nafikiria product ninayotengeneza itasaidia ngozi aina gani.

Afroswagga – turudi katika mitindo ulianza kama mwanamitindo je ile nafasi bado ipo utarudi au ndio basi tena?

Nuya – Hahahah kwa kweli nafasi ipo kama itatokea, bado napenda uanamitindo bado, japo kwa sasa mambo yameanza kuwa mengi ila nikiwa free why not?! Kama mwaka jana, nilikuwa Model wa Bijoux Trendy kwenye Swahili Fashion Week, Nilikuwa na wakati mzuri sana.

Afroswagga- tunakuona una pendeza japo upo simple je nini huwa kinakujia akilini wakati una plan a outfit?

Nuya -Inategemea siku hiyo ninaenda wapi au nina kazi gani. Naishi Zanzibar, kwa hiyo mavazi yangu yako simple, magauni kama ni easy day au kama niko kazini ni jeans na tshirt.

Afroswagga – tumeona N.E bags ni product mpya? na tutegemee nini kingine kutoka N.E?

Nuya -Ndio, NE. Everyday Tote Bags ni product yetu mpya ambayo nimeshirikiana na designer wa nyumbani Bijoux Trendy. Kuna Bidhaa mpya nyingi zinakuja kwa hiyo tukae mkao wa kula.

Afroswagga -Tutegemee maduka ya N.E bara pia au tuzifuate tu huko huko Zanzibar?

Nuya – Kwa sasa tunapatikana Stone Town, Zanzibar. NE. shops zitakuwa mikoa michache na baadhi ya miji mikubwa barani Africa na hata nje ya Africa.

Afroswagga – Chochote ambacho ungependa kuwaambia wa Tanzania kuhusu N.E

Nuya – Napenda kuwashukuru sana watanzania kwa kunipa support tokea nimeanza mpaka hapa nilipo, nashukuru Mungu kwa kunipigania na kunisimamia kwenye changamoto nyingi sana ambazo nimepitia kuijenga Nuya’s Essence, safari bado ni ndefu sana lakini ninaamini tupo pamoja na tutakuwa pamoja. Kwa vijana wanaosoma haya mahojiano, kamwe usiruhusu mtu kukwambia huwezi jambo Fulani. Pigani ndoto zako, Sali sana na uwe karibu na Mungu hakika utafanikiwa. Ahsante sana Afro swagga kwa hii platform ya kushare maisha yangu na biashara yangu na waTanzania mbarikiwe sana.

Kama ungependa kupata bidhaa za Nuya Mtafute Hapa @nuyasessence 

Aksanteh Kwa Ushirikiano Wako

 

Related posts

6 Comments

 1. buy golden teacher mushroom online tool,

  … [Trackback]

  […] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-na-kupata-skin-tips-kutoka-kwa-hellen-dausen-nuyas-essence/ […]

 2. click here for more info

  … [Trackback]

  […] There you will find 81404 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-na-kupata-skin-tips-kutoka-kwa-hellen-dausen-nuyas-essence/ […]

 3. test Automation Tools

  … [Trackback]

  […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-na-kupata-skin-tips-kutoka-kwa-hellen-dausen-nuyas-essence/ […]

 4. Study Medicine in Nigeria

  … [Trackback]

  […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-na-kupata-skin-tips-kutoka-kwa-hellen-dausen-nuyas-essence/ […]

 5. unicc alternative

  … [Trackback]

  […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-na-kupata-skin-tips-kutoka-kwa-hellen-dausen-nuyas-essence/ […]

 6. สล็อตเว็บตรง

  … [Trackback]

  […] There you can find 16854 more Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/pata-kumjua-na-kupata-skin-tips-kutoka-kwa-hellen-dausen-nuyas-essence/ […]

Leave a Reply