Anaitwa Saleh Hamimu, Kijana wa miaka 20 ambae amejikita katika ubunifu. Amesha wavalisha mastaa mbali mbali akiwepo Mtangazaji wa storm tv Liliane Masuka, Mtangazaji Tahiya George ambae ame top list yetu ya waliopendeza katika event ya Sultan Fore Men Launch lakini pia amemvalisha Miner Spartan. Tumepata kuketi nae na kujua mawili matatu kutoka kwake.
Afroswagga – Saleh Ni Nani Hasa?
Saleh – Naitwa Saleh Hamimu… Ni Kijana Wa Wa Miaka 20, Mbunifu, Mtafutaji, Mcheshi Na Mwenye Heshima Kwa Wakubwa Na Wadogo…Nimemaliza Elimu Ya Msingi Mkoani Mtwara Na Kuendelea Na Sekondari Jijini Dar Es Salaam…Ni Mtoto Wa Nne Katika Familia Ya Watoto Sita…
Afroswagga- Nini Kimevutia Katika Fashion?
Saleh – Napenda Sana Fashion, Ni Kitu Kitu Ambacho Kipo Ndani Yangu…Baada Ya Kugundua Nina Kipaji Cha Ubunifu Nikaona Ni Bora Nitumie Nguvu Na Akili Nyingi Kwenye Tasnia Hii…Kufanya Kitu Ambacho Unakipenda Ni Rahisi Kuliko Fani Amabayo Hauipendi…
Afroswagga -wewe ni mwanaume na una buni nguo za kike, unapata wapi inspiration?
Saleh – Nadhani Mtu Ukiwa Na Kipaji Unaweza Kukionyesha Kwa Njia Nyingi, Mfano Mzuri Ni Barnaba Ambae Huwa Anaandikia Nyimbo Wasanii Wengi Wa Kike Kama Linah, Shilole,Luludiva Na Wengineo…
Inspiration Napata Kwa Watu Wengi,Kwa Nchini Tanzania Namuangalia Elizabeth Michael (Lulu) She Has The Sweet Fashion Taste We All Need…Nje Ya Tanzania Ni Rihanna Ambae Anajaribu Vitu Vingi…
Afroswagga – mpaka sasa feedback ya uliyo wavalisha ipoje?
Saleh – I Must Say Feedback Ni Nzuri Sana Kutoka Kwa Wateja Wangu Wengi Niliowavalisha…Wamekuwa Wakinipongenza Na Kufurahia Nguo Zao…
Afroswagga – kama up coming unawezaje kuwavalisha waatu maarufu?
Saleh -Nadhani Kuvalisha Watu Maarufu Ni Uwezo Wa Mtu Kujaribu Kuomba Kufanya Kazi Nao…Baada Ya Kufanya Kazi Na Liliane Masuka Mtangazaji Wa Kipindi Cha Storm (Clouds) Ilinipa Wigo Mkubwa Wa Kufanya Kazi Na Watu Wengine Wengi…
Afroswagga – nani ambae ungependa kufanya nae kazi siku moja na kwanini?
Saleh – Napenda Na Ningefurahi Kufanya Kazi Na Elizabeth Michael (Lulu) Kama Nilivyosema Ana Fashion Taste So Everything She Puts On Looks Effortless Beautiful On Her…Nampenda Sana And I Think She Has Something That Always Commands Adoration…
Afroswagga – utakua unawalisha tu watu maarufu? kuna collection zinakuja au tutegemee nini kutoka kwako?
Saleh – Hapana, Sitokuwa Navalisha Watu Maarufu Tu Ila Kwakuwa Watu Maarufu Ndo Ambao Zinaonekana Kwa Watu Wengi Ndiyo Maana Zinaonekana Sana Kazi Zao…Kuna Collection Mpya Ambayo Its Still In Making Kwahiyo Watu Wasubiri Vitu Vizuri..
Afroswagga – mtu akitaka bidhaa yako/kazi yako anaweza kukupata vipi?
Saleh – Kwa Anaehitaji Bidhaa Zangu Apitie Kwenye Ukurasa Wangu Wa Instagram @Officialsalehamimu Atapiga Na Kupata Maelezo Yote…
Afroswagga – chochote ambacho ungependa kuwaambia wa Tanzania
Saleh- Nawapenda Sana Na Nashukuru Kwa Kupokea Kazi Zangu Vizuri…
kupata interview nyingine na nancy owner wa own look bonyeza hapa
Related posts
HOT TOPICS
We need to have some sort of bima ila for enjoyment. Yaani wanakata ka % ka mshahara kako unakua na card ukienda se… https://t.co/W9oDoaN2YY
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…