Ikiwa tunaelekea Miss Tanzania 2019, ambayo itafanyika tarehe 23/8/2019 tumeona tutoerai kwa miss Tanzania ya nini cha kujifunza kutoka kwa Amber Lulu Na Zari The Bosslady.
Julai 14 kulikuwa na mashindano ya Miss Kinondoni 2019, ambapo mtumbuizaji alikuwa mwanamuziki Amber Lulu huku Hamisa Mobetto akiwa judge katika event hio. Hatujui kama walikuwa wana makwazo tangu zamani, ni utani au kiki lakini Amber alipanda kwenye stage na kuanza kumuongelea Hamisa Mobetto vibaya mbele ya kadamnasi tena ikiwa sherehe ya kumtafuta mrembo wa Kinondoni 2019.
Hali hii ikaja kuonekana Uganda tena ikiwa ni siku chache tu tangu Amber Lulu afanye sakata hilo, mwanadada Zari The Boss Lady alimshambulia mshereheshaji wa event ya Miss Uganda 2019 Anita Fabiola na yeye akiwa mbele ya kadamnasi tena basi mbele ya Miss World na Miss Africa (shame)
View this post on InstagramA post shared by MATANGAZO YA BIASHARA NJOO DM (@bongostar5_habari) on
Nini tujifunze au kurekebisha kutokana na haya matukio mawili tukiwa tunaelekea Miss Tanzania 2019
- Tutafute professional people
Kuanzaia washereheshaji, mc na ma judge wote ambao wana professional ya kujudge ma miss na kujua hapa ni pakuongea nini ( ku-set aside any difference ambazo wanazo na kufanya kazi). Inapokuwa sio professional yako huoni uzito wa hilo swala na kuishia kutia aibu Nchi na watu wake. Tuachane na nani ana kiki kwa wakati huu na kutafuta watu ambao wapo serious ambao watatulete matokeo mazuri.
Kuwapa kazi watu ambao hawajui uzito wa hili swala matokeo yake ndio haya na yeye anataka atafutie kiki hapohapo aongelewe badala ya kufanya kazi yake shughuli ikaenda vyema. Hatuhitaji kuleta watu kutoka Nje tuna watu wengi wengi wanaojua wanacho kifanya, wapo kwenye industry kwa miaka mingi na wanajua uzito wa Miss Tanzania na heshima yake.
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/rai-yetu-kwa-miss-tanzania-2019/ […]