SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Rangi Za Suit Unazoweza Kuvaa Mwanaume Ukiachana Na Nyeusi Na Navy Blue
Mitindo

Rangi Za Suit Unazoweza Kuvaa Mwanaume Ukiachana Na Nyeusi Na Navy Blue 

Wanaume wengi hawapendi kuvaa mavazi yenye rangi rangi mara nyingi rangi zao wao ni zile zilizopoa hasa hazina kelele nyingi, Kwa upande wa vazi la suit wanaume hupendelea kuvaa rangi nyeusi, navy blue, khakhi au rangi nyingine zilizopoa lakini kumbe inawezekana wao kuvaa rangi za kuonekana kidogo japo si kushout sana kama soft pastel colors.

Katika pitapita zetu tumekutana na baadhi ya watu maarufu wa kiume wamevaa suit zenye rangi kidogo na zikatuvutia kuwaletea na ninyi hapa uka pata idea ya rangi ipi unaweza kuongezea katika kabati lako la suit.

Tulimuona Harmonize akiwa amevalia  suit ya blue kutoka kwa mbunifu Martin kadinda, kumalizia hii suit Harmonize alivaa shirt nyeupe kwa ndani na viatu vyeupe, amemalizia na ku accessorize na miwani, saa na hereni.

  • tumependa kuona Harmonize amepewa muonekano wa tofauti kama ambavyo tunajua Harmonize ana dark skin color, anahitaji kuvaa vitu ambavyo vinarangi kudogo ili kufanya a-pop, the color fits him well na jinsi ambavyo amekuwa styled ni perfect.

Msanii kutoka katika kundi la The Mafiki, Mbalamwezi acoustic tulimuona akiwa amevaa suit kutoka kwa mbunifu Ki2pe ambayo ilikuwa na rangi ya peach, tumependa rangi ya hii suit japo ina rangi kidogo lakini imetulia, tunatamani wange i-style vizuri zaidi ya hapa sababu kama wameishusha hivi ukali wake kwa kui-style vibaya. Rangi nzuri suit imeshonwa vizuri unaweza kustyle na shirt jeupe au jeusi ikapendeza zaidi.

Msanii na muigizaji Romeo yeye tulimuona akiwa katika pink suit, he looked dapper. tumependa alivyo ivaa na rangi ambazo zipo calm zaidi kuliko suit kama ungependa kufanya rangi ya suit yako isipige sana kelele unaweza kuivalia na neutral colors kama ambavyo Romeo amefanya hapa.

Rapper Jay Z na yeye alionekana akiwa amevali suit ya rangi ya kijani, akiwa amestyle na chain kubwa ya gold.

Kama ambavyo mmeona Pastel suits are in, unaweza kuvaa kwenye meetings, red carpet au hata katika sherehe mbalimbali, uta stand out na kuonekana wa tofauti. Usiogope kujaribu rangi unacho takiwa kujua ni ngozi yako inaendana na rangi gani na unawezaje kustyle rangi hizo bila kupiga kelele.

Related posts

4 Comments

  1. เครื่องคอริ่ง

    … [Trackback]

    […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/rangi-za-suit-unazoweza-kuvaa-mwanaume-ukiachana-na-nyeusi-na-navy-blue/ […]

  2. Liberty Caps Mushroom

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/rangi-za-suit-unazoweza-kuvaa-mwanaume-ukiachana-na-nyeusi-na-navy-blue/ […]

  3. Buy Mushroom Online Melbourne

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/rangi-za-suit-unazoweza-kuvaa-mwanaume-ukiachana-na-nyeusi-na-navy-blue/ […]

  4. window installer

    … [Trackback]

    […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/rangi-za-suit-unazoweza-kuvaa-mwanaume-ukiachana-na-nyeusi-na-navy-blue/ […]

Comments are closed.