SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Reviewing Bongo Star Search Red Carpet Looks
Mitindo

Reviewing Bongo Star Search Red Carpet Looks 

Siku ya jumanne kuamkia jumatano ambapo ulikuwa mkesha wa Christmas, shindano na bongo star search 2019 lilifikia taamati ambapo tulipata mshindi ambae ni Meshack Fukuta.

Well wakati wengine walikuwa wanaangalia kujua nani atachukua ushindi sisi tulikuwa tukiangalia nani alivaa nini na hizi ndio two cents zetu katika mionekano ya siku hiyo.

Tuanze na chief judge ambae ni Rita Paulsen wengi tunamjua kama madam Rita, Rita alivaa metallic blush pink ball dress, we love the design, kifuani na mikono ilikuwa perfect ambacho hatukukipenda ni material ya hii nguo imefanya nguo ionekane mbaya na somehow cheap. Makeup, hair & accessories zilikuwa on point.

Judge mwingine ni Lady Jay Dee ambae yeye alivaa sequin sheer dress, tulipenda kwamba alichagua nguo fupi lakini ina make statement, the shoes & makeup zilikuwa on point ambacho hatukukipenda ni nywele the hair ruin the look imeonekana too much with the accessories on it issa NO. Tunatamani angeweka a simple bun bila makorokoro.

Hatujui kama judges walipania sana au vipi, Master Jay alivaa hii check suit ambayo kama ingevaliwa vyema angependeza sana, throw the tie away, throw hizo shoes na apate a classic shoes kama Oxford au Moccasin’s.

Idris Sultan showed up in agbada, we love the color & style tunatamani angetoa hio kofia imefanya the look isiwe na coordination but otherwise Idris alijitahidi.

Muigizaji Ebitoke na yeye alihudhuria katika onyesho hili, we love the makeup & hair. Gauni ni nzuri sana lakini haikuwa kwa mwili wake waswahili tunao msemo unasema “mjusi ndani ya gogo” basi ndivyo ambavyo Ebitoke alionekana.

Washiriki wa BSS wakiwa katika red carpet, lets say we love few look and few were just abomination

Related posts