Gigy Money amesheherekea Birthday yake Ijumaa ambapo ametimiza miaka 26 na akiwa ametimiza miaka 10 katika industry ya mziki.
Kama ilivyo kawaida Gigy aliandaa Birthday Photoshoot akiwa ame-serve looks kadhaa na tupo hapa ku-review looks hizo,
Look ya kwanza ni hii blue ballgown yenye white shirt & tie huku chini ikiwa attached na sculptural rosettes, hii alipendeza sana na hii look makeup on point, neat hair style.


Kitu kikubwa tumeona ni kwenye mitandao ya kijamii ikiwa inafananisha hili vazi na lilovaa Cardi B katika Met Gala 2023, which ni kweli wamekuwa inspired huko, tatizo tuliloliona ni material ime disappoint na kwamba maua ni machache mno na chini haikutuna vizuri, fabric ni laini ime drape badala ya kukamaa (lol), tuliona Sandra kutoka Nigeria alikuwa Inspired na ikatokea vyema kutokana na kwamba walitumia maua mengi tunadhani wangepata fabric nzuri au maua yangeongezwa zaidi ingekaa vyema zaidi.


Look ya pili ilikuwa hii dramatic sculptural blue dress ambayo ilikuwa na cutouts pembeni huku ikiwa imebuniwa kuwa na corset sehemu ya kifuani na tumboni, gauni ilo lilimaliziwa likiwa limeunganishwa na dramatic train pieces zilizopitia kichwani na mabegani, well alipendeza mno pia kila kitu kilikaa mahala pake.


Hii look pia ilikuwa inspired na Cardi B ambapo alivaa hii gauni katika tuzo za Grammy 2023, tuliiona pia kwa m-Nigeria Naomi Silenokula akiwa na yeye amejaribu kuiigia kama ya Cardi.


Tumeona namna gani mbunifu Rakel amejitahidi ku-recreate hizi looks huku akijaribu kuweka touch’s zake, sote tutakubaliana kwamba amejitahidi sana na tunaona bright future kwake, kwetu tungependa kumwambia akazie alipo lakini pia ajaribu kutafuta materials zitakazo kuwa bora zaidi na pia sio lazima ku-recreate mavazi anaweza kubuni yake akaleta utofauti.
Pia kama ata re-recreate vazi lingine basi ajaribu liwe kama ambalo ameliona au zaidi kwasababu uki re-recreate kitu halafu ubora ukawa pungufu unajiharibia jina na kuwa unaongelewa mtandaoni na hii itashusha brand, so next time jitahidi kuwa on point au pitiliza malengo in a good way all in all unakitu utafika mbali
Credits dress by @rackel_stylish
Makeup @lucytouches
Hair @jonijohairtz
Picha ya Rais wa vichaa wote @chizimapicha
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…