SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Reviewing Looks From Barnaba & Raya’s Wedding
Mitindo

Reviewing Looks From Barnaba & Raya’s Wedding 

Mwanamuziki Barnaba amefunga ndoa na mkewe Raya, wawili hawa walifunga ndoa ya kiislam, walikuwa na sherehe 3 ambapo ni send off ndoa na wakamalizia na reception na tupo hapa kuangalia mavazi ya sherehe zote tatu.

Kwenye ndoa Barnaba alichagua gold and white, ambapo alivaa kanzu nyeupe akamalizia muonekano wake na cream kimono chenye nakshi za gold, belt ya gold aliyo-match na kitambaa kichwani huku Raya yeye akiwa amevalia baby blue look, top na skirt ya blue yenye embellishement za gold akamalizia na mkufu wenye blue na vail yenye blue na gold.

Send off Raya alikuwa na looks mbili ambapo aliingia na hii pink dress na muonekano wa pili ulikuwa ni gold corset, Baranaba yeye alikuwa amevalia two pieces nyeupe zenye nyeusi kwa mbali akamalizia muonekano wake na miwani pamoja na viatu vyeusi.

Tunadhani Barnaba alikuwa simple kumpa Raya nafasi ya ku-shine maana ilikuwa siku yake.

Reception wote walikuwa na looks mbili ambapo waliingia na hii ya kushoto, white mermaid dress yenye urembo chini na huku Barnaba akiwa kwenye blue suit, na look ya pili ilikuwa ni hii white pencil pearled dress huku Barnaba akiwa na purple suit.

Walipendeza tumependa kwamba Barnaba amebana nywele zake vyema, tumependa hakuweka zile wallets zake zinazotunisha mifuko kwenye suruali amekuwa neat.

Well Mavazi yote ya Raya kasoro la siku ya ndoa yanatoka kwa @designed_by_shuu

Nails 💅🏻 @thebossnailstz

Makeup @jodees__makeup / @rosekayuga__

Headpiece @weavefairytz

Hair @sephahair_clinic

Blue Suit Ya Barnaba Inatoka Kwa @mtani_bespoke

Purple Suit Ya Barnaba Inatoka Kwa @sutibega_

Send Off Outfit Ya Barnaba Inatoka Kwa  @kanzuland

📸 @chumbachu_ / 📷 @icon_tz

Hongera kwa Maharusi na Tupe Maoni Yako Hapo Chini Look Ipi Umeipenda Zaidi?

Related posts