Nani ambae ana heart break na haijui huu wimbo? wimbo una trend na unagusa wengi, kama wengine mimi nilikuwa mmoja ya watu ambao walikuwa wanasubiri hii video itoke, kiukweli ime ni-disappoint kidogo nilijua itakua more of dancing video ila director kaamua kupita kushoto, sio mbaya kuwa tofauti anyways hayo sio yaliyo tulita hapa leo tupo kuongelea looks za kwenye hii video.
Tuanza kusema kwanza looks za wadada ni moto sana, color co-ordination zao nzuri, fitting nzuri, nywele na makeup zimetulia very nice na zinaishi sio trendy fit sana yaani unaweza kuiangalia video mwakani na bado ukaona wanamionekano mizuri
Suit za apperances kwa mujibu wa Rayvanny alizinunua kwa 200,000/- na walikuwa watu 200 alitumia 40,000,000 kwaajili ya mavazi hayo, tunaweza kusema ni investment kubwa & walijitahidi kupendeza .

Tuanze na Rayvanny tunataka kusema Ray aanze kuujulia mwili wake nini unataka na nini hautaki as yeye ni mfupi na ana mwili anapendeza sana akivaa fitted cloth kwenye hii video nguo nyingi ni oversized ameonekana kuwa mpana zaidi.
Kingine pale alipovaa magwanda alitakiwa kujaribu kuvaa na viatu vya kawaida boots zimemmeza na kumfanya azidi kudidimia au kuonekana mfupi zaidi, vingine ni sawa kwetu hasa kwenye nywele na accessories

Kwa Diamond tumeona mavazi ni sawa hayana tatizo japo ni repeatition kasoro rangi za nguo na location kikubwa ni accessories tumeona aliamua kuvaa mikufu yake yote which was kinda too much kwenye macho yetu.

Tupe maoni yako hii video wewe umependa na kutopenda nini upande wa fashion
Related posts
HOT TOPICS
We need to have some sort of bima ila for enjoyment. Yaani wanakata ka % ka mshahara kako unakua na card ukienda se… https://t.co/W9oDoaN2YY
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…