SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Reviewing The Kid You Know Album Release  Looks
Mitindo

Reviewing The Kid You Know Album Release Looks 

Jumamosi iliyopita ilikuwa album release ya msanii Marioo, ambapo aliamua kufanya event pale Mlimani City na kuhudhuriwa na watu maarufu na fans wake. Well kama kawaida yetu tuliangalia nani amevaa nini na Je kapendeza au lah?

Bado tunaona kuna tatizo la kujua cha kuvaa kutokana na event husika nadhani tumezoea sana ma event makubwa kiasi ambacho tunasahau kwamba kuna event unavaa tu simple mfano mzuri ni hii event ilihitaji nguo simple nzuri na sio miburuzo. Tuone walio itendea haki event

Tunaanza na Gigy Money, Gigy alielewa assigment tumependa hii short dress yake nyeusi yenye statement sleeves, shoes, makeup on point anaweza kunyanyuka akacheza bila kukanyagwa au kusumbuliwa na vazi kulinyanyua nyanyua. Gigy amevalishwa na @michaelwilliams.x , Hair @jonijohairtz ,Makeup @shamayssalo, Picha @chizimapicha ðŸ’˜

Elizabeth Michael as usual mama G huwa anajua afanyalo tumependa hii short pant suit, makeup yake nae ilikuwa on point & hair style nzuri the look is class & comfortable, Eliza amevalishwa na Suit @jm_international_collection, MUA @jodees__makeup , 📸 @chizimapicha

Aunty Ezekiel, Amejitahidi na hii look japo tunadhani angechagua rangi nyingine angependeza zaidi hii nyeupe somehow inatupa bridal shower vibes but all in all kigauni kilimpendeza na hakuvaa miburuzo Aunty amevalishwa na @designed_by_shuu ,Pic by @kenlaw_photography

Mrs Bill Nas, Nandy nae alikuwepo yeye alivaa hii embellished velvet short dress akamalizia look yake na mettallic boots, alipendeza pia ameendana na event lakini pia ifike mahala tujue kupunguza urembo kwenye mavazi na kujua urembo gani unaendana na urembo upi ili tusilete confusion kwenye vazi. Hair & MUA @makeupbyeddie_, Dress @rackel_stylish

Hamisa Mobetto alikuwa in all black look, Hii look ya Hamisa imetuwazisha sana kureview kuna kitu hakipo sawa tunadhani kuna vitu vitatu vinaleta utata na ni nywele, viatu au hii extra skirt ya chini endapo angerekebisha kimoja basi angetisha zaidi.

Kajala Masanja in black & gold look, hii dress ni nzuri sana tungependa zaidi kama ingekuwa fupi au ingekuwa pensil zaidi ila amependeza

Abby Chams yeye aliamua kuvaa co-ord

Kwa wanaume tumeona wengi wao wamevaa vyema kuendana na event tunajua wanaume huwa hawanaga mbwembwe nyingi, wengi wao walikuwa na suit which zimewapendeza mno, tumewaona Juma Jux, BillNas na B Dozen looking Sharp

Bill Nas

B Dozen

Tupe maoni yako ni nani ametisha zaidi kwenye hii list

Related posts

2 Comments

  1. Plantation Shutters

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/reviewing-the-kid-you-know-album-release-red-carpet-looks/ […]

  2. goldendoodle puppies

    … [Trackback]

    […] Here you will find 8896 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/reviewing-the-kid-you-know-album-release-red-carpet-looks/ […]

Comments are closed.